Thursday, January 16

KAMISHENI ya Utalii Pemba, wanafunzi wa skuli ya Madungu Sekondari na wafanyakazi wa Pemba Lodge waufanyia usafi ufukwe wa Kisiwa cha Shamiani Mwambe

NA ABDI SULEIMAN.

KAMISHENI ya Utalii Pemba, imesema kuwa lengo la kufanya usafi katika ufukwe wa Kisiwa cha Shamiani Mwambe, ni kuutangaza ufukwe huo kuwa moja ya vivutio vya utalii vilivyopo Kisiwani Pemba.

Kauli hiyo imetolewa na Mdhamini wa Kamisheni hiyo Hamad Amini, wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ufanyaji usafi katika fukwe hiyo, kwa kushirikiana na watendaji wa kamisheni, wanafunzi wa skuli ya Madungu Sekondari na wafanyakazi wa Pemba Lodge.

Alisema ufukwe huo ni moja ya fukwe muhimu na nzuri katika kisiwa cha Pemba, kuliko ufukwe wa vumawimbi ambao umezoeleka kutumiwa na wananchi.

Alisema bado ufukwe wa Shamiani Mwambe haujajulikana, nifukwe safi na yakuvutia wawekezaji, hivyo kamisheni imelazimika kufanya usafi ili kuutangaza.

“Pemba tume jaaliwa kuwa na fukwe nzuri na za kuvutia, ni maeneo ya watu kupumzika bila ya matataizo yoyote, chamsingi kufuatwa taratibu tu”alisema.

Aidha alisema wakati umefikwa kwa wawekezaji kuekeza ktika kisiwa hicho, kwani wageni wengi wataweza kuvutiwa na ufukwe huo, kutokana hali yake ya hewa nzuri.

Akizungumzia changamoto iliyopo, alisema lazima usafiri wakufika kisiwani huko kutumia kwa usafiri wa boti, jambo ambalo serikali inapaswa kuweka boti ya kisasa katika kisiwa hicho.

Meneja wa Pemba Lodge shamiani Mwambe Massoud Ali Hamad, alisema kisiwa cha Pemba kimejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya kiutalii, ikiwemo fukwe nzuri za kuvutia.

Alisema baadhi ya wageni wanaofika katika kisiwa hicho, huvutiwa na mazingira ya kisiwa na ufukwe wake mkubwa nab ado uko katika mazingira mzuri.

Aidha aliiyomba serikali kuvitangaza vivutio vya kiutalii vilivyopo ndani ya kisiwa hicho, ili wageni waweze kupatikana na kuongeza pato la taifa.

Naye Mtembeza watalii kisiwani Humo Hmweji Hija Makame, alisema hoteli ya Pemba Lodge ilianzishwa mwaka 2001 hadi sasa inavyumba nane vya kulala wageni.

Naye Mwanafunzi Amour Shaame alisema fukwe badi iko vizuri inavutia, wala haijaharibiwa kama ufukwe wa vumawimbi, serikali inapaswa kuutanga zaidi ufukwe huo.

Kwa upande wake Wahda Hamad Ali, alisema ili watalii waweze kufika katika kisiwa hicho, wanapaswa kutunza mazingira yaliyomo ndani ya kisiwa hicho, ikiwemo ufukwe huo kuendelea kuwa safi ili watalii wakija wataweza kuongeza kipato cha nchi.

Mwanafunzi Mwengine Maryam Mansour Rashid, aliyombo serikali kuweka mkazo zaidi katika suala la usafiri, wa kisasa kufika kisiwani huko, kwa lengo la kutembelea vivutio vilivyoko huko na kuanza kuonekana.