Saturday, January 18

Rais Dk Hussein Mwinyi afanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya “International Holding Company “ (IHC) ya Abu Dhabi

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya “International Holding Company” (IHC) ya Abu Dhabi  Bw.Syed Basar Shueb (katikati) akiwa na Ujumbe wake  akisoma kitabu cha muongozo wa Uekezaji Zanzibar, wakati wa mkutano wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa kampuni hiyo Abu Dhabi leo 18-1-2022.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya “International Holding Company “ (IHC) ya Abu Dhabi ukingozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.Syed Basar Shueb, kuzungumzia masuala ya Uwekezaji Zanzibar, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kampuni hiyo Abu Dhabi leo 18-1-2022, na (kushoto kwa Rais) Balozi wa Tanzania (UAE) Mhe. Balozi Mohammed Abdalla Mtonga.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya “International Holding Company “ (IHC) ya Abu Dhabi ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.Syed Basar Shueb, kuzungumzia masuala ya Uwekezaji Zanzibar, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kampuni hiyo Abu Dhabi leo 18-1-2022, na (kushoto kwa Rais) Balozi wa Tanzania (UAE) Mhe. Balozi Mohammed Abdalla Mtonga na (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Bw, Shariff Ali Shariff.(Picha na Ikulu)

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw.Shariff Ali Shariff akizungumza na kutowa maelezo ya fursa za Uwekezaji Zanzibar ,wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto ) na Uongozi wa Kampuni ya “International Holding Company” (IHC) ya Abu Dhabi ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.Syed Basar Shueb.na (kushoto kwa Rais) Balozi wa Tanzania Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.Mhe. Balozi Mohammed Abdalla Mtonga.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya “International Holding Company “ (IHC) Bw. Syed Basar Shueb akizungumza  katika mkutano huo kuhusiana na fursa za uwekezaji Zanzibar katika sekta mbalimbali za uchumi, uliofanyika katika ukumbi wa Kampuni hiyo Abu Dhabi leo 18-1-2022.(Picha na Ikulu)