Monday, November 25

Wajasiriamali kisiwani Pemba waishukuru serikali kuwapatia mikopo

Wajumbe wa Kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi wakikagua mradi wa ufugaji wa Ngombe katika kikundi cha Tundwa Coperative Society ambacho kimenufaika na Mkopo unaotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Wajumbe wa Kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi wakikagua mradi wa ufugaji wa Ngombe katika kikundi cha Tundwa Coperative Society ambacho kimenufaika na Mkopo unaotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Wajumbe wa Kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi wakikagua wajasiriamali wa  mradi wa utengezaji majiko sanifu huko ukunjwi  Chanjaani ambao wamenufaika na Mkopo unaotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Na Massoud Hamad, BLW

Wajasiriamali kisiwani Pemba wamesema hatua ya serikali kuwasaidia kuwapatia mikopo kumewawezesha kusongesha mbele maendeleo endelevu na kupunguza umaskini kisiwani humo.

Wamaeeleza hayo kwa nyakati tofauti wakati walipotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi kujionea namna wajasirimali hao walivyoweza kunufaika na mikopo hiyo.

Wamesema kupitia mikopo  wanayopatiwa ambayo haina vikwazo vikubwa imewawezesha kubuni shughuli mbali mbali za kiuchumi na kutoa ajira kwa vijana wengine kupitia miradi waliyoianzisha ikiwemo ya kilimo, ufugaji na biashara.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi Na Uwekezaji Mhe Mudrik Ramadhan  Soraga amesema kutokana na hatua kubwa za  maendeleo ya wajasiriamali hao kupitia mikopo hiyo ipo haja ya kuwaongezea ili kuweza kuwagusa watu wengi zaidi.

Nao wajumbe wa Kamati ya Uchumi chini ya Mwenyekiti wake mhe Sabiha Fil fil Thani wameishauri wizara kuendelea kutoa kipaombele cha kuwapatia  mikopo na vitendea kazi wajasiriamali ambao wanafanya shughuli zenye tija ili waweze kurejesha kwa wakati na kuwanufaisha wengine.