Na Raya Hamad – OMKR
Imeelezwa kuwa sheria mpya ya Watu wenye Ulemavu inayokuja itahakikisha kuna kipengele kinacholazimisha kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakaemficha mtoto au mtu mwenye ulemavu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kipindi cha Octoba hadi Disemba 2021, mbele ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa katika Ukumbi mdogo wa mkutano Gombani.
Dkt Saada amesema Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu katika kuyatafutia ufumbuzi changamoto za Watu wenye Ulemavu limefanya ziara mbali mbali kusikiliza changamoto, vikwazo na malalamiko ya walengwa kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi likiwemo baadhi ya wanajamii kuwaficha watoto wenye ulemavu na kuwakosesha haki zao za msingi
Aidha Ofisi yake imeanza kutoa mafunzo ya lugha ya alama kwa watendaji wa Serikali kutoka taasisi 17 kwa ajili ya kuwapatia taaluma ili Watu wenye Ulemavu wa Uziwi waweze kuhudumiwa bila kipingamizi wanapohitaji huduma kutoka kwenye taasisi zote za Serikali na binafsi
Akizungumzia kuhusu suala la miradi iliyofanyiwa tathmini za athari za kimazingira Dkt Saada amesema baada ya kufanyika tathmini hio kwa miradi ya maendeleo ya kiuchumi hutolewa vyeti vya mazingira na masharti yay a kimazingira ambayo husaidia kupunguza uharibifu na uchauzi wa mazingira na kuifanya miradi kuwa endelevu
Pia Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ZEMA imefanya ziara ya kufatilia mazingira kwa miradi saba 7 ya kiuchumi na matokeo ya ziara hizo ni kuongezeka kwa mwamko wa wawekezaji katka kudhibiti athari za kimazingira kwenye miradi yao
“mambo makubwa yaliyobainika kwenye ziara hizo tumeona Hoteli nyimgi zimeanza kuzingatia masuala ya kimazingira ikiwa ni pamoja na kutenganisha taka za kuoza na zisizooza, kuimarisha maeneo ya kimazingira na kudhibiti maji machafu” alilisistiza Dkt Saada
Kuhusu Dawa za Kulevya Dkt Saada amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inashirikiana na Mamlaka mbalimbali za Serikali katka mapambano dhidi ya Dawaza Kulevya zikiwemo Jeshi la Polisi, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Mahakama hususan katka masuala mbalimbali yanayohusiana na udhibiti na uchunguzi wa kesi za Dawa za Kulevya.
Dkt Saada pia ameiyambia Kamati hio kuwa Tume ya UKIMWI ambayo ina jukumu la uratibu, ufatiliaji na tathmini juu ya muitiko wa Taifa wa UKIMWI na mawasiliano na utetezi wa masuala ya VVU na UKIMWI katika kipindi cha Octoba hadi Disemba 2021 pamoja na mambo mengine imeratibu na kusimamia kampeni za kijana kataa UKIMWI
Kufanya ziara za ufatiliaji na tathmini kwa vituo vinavyotoa huduma za UKIMWI (CTC) vya Hospitali ya Abdalla Mzee, Chake Chake, Micheweni na Wete pamoja na vituo vya huduma rafiki Mkoani, Mbuzini, Bwagamoyo na ZAYEDESA Mkoani Pemba
Aidha Tume ya UKIMWI imefanya mikutano uliwashirikisha wadau 25 kwa lengo la kutoa maoni juu ya maandalizi ya mpangp Mkakati wa Mapambano dhidi ya UKIMWI, jumla ya taasisi 12 zilitembelewa kwa lengo la kukusanya maoni juu ya maandalizi ya mkakati huo wa 5 wa UKIMWI
Akielezea changamoto Dkt Saada amesema kumekuwa na ongezeko kwa tabia hatarishi kwa vijana na jamii hata hivyo kampeni mbali mbali za elimi ya kinga kuhusu UKIMWI inaendelea kutolewa kwa ujumla pamoja na ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU
Upungufu wa baadhi ya watumishi wa Idara na Taasisi za Pemba ikiwemo Ofisi ya Faragha ambapo kwa sasa wameazima kutoka taasisi nyengine, kukosekana kwa jengo la Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba ambapo tayari jitihada zinaendelea za kutafuata jengo kwa ajili ya Ofisi Kuu
Nae mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mhe Hassan Hafidh ameiomba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuharakisha kuzifanyia marekebisho sheria zote zilizobakia ikiwemo ile ya UKIMWI na Watu wenye Ulemavu na Mazingira ili mabadiliko ya kiuchumi yaendane na sheria za nchi kwa maslahi ya Taifa na wananchi
Mhe Hassan pia ameishauri Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais pamoja na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha magari yanayowachukuwa viongozi wa Kitaifa wakati wakiwa kwenye misafara yawe mazima na yawe yanamilikiwa na Serikali sio binafsi ama taasisi binafsi kwa maslahi ya nchi