NA SAID SAID NGUYA – OFISI YA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewahakikishia wanachama na wananchi kwa ujumla kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha, kila kilichoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020 – 2025, kitatekelezwa kwa kiwango chenye tija.
Katibu Mkuu ameyasema hayo leo Jumatatu, Januari 24, mwaka huu, alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho katika maeneo tofauti Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya za Wete na Micheweni katika ziara maalum ya siku mbili akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
“Niwahakikishe Chama Cha Mapinduzi kimejipanga, kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020- 2025 ambayo imeahidi mambo mbalimbali ikiwemo maji, umeme, barabara,
miundombinu ya elimu…imeahidi mambo mengi ndani yake, inatekelezwa kwa kiwango chenye tija.”
“Ndiyo maana mnaona tunapita kama hivi. Kazi yetu sisi ni kupita kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa tulichokiahidi kwenu, na ndio kazi tunayoifanya sasa hapa Pemba kwa siku mbili,” amesema Katibu Mkuu Ndugu Chongolo akizungumza na wanachama na wananchi wa Kijiji cha Taifu, baada ya kuweka jiwe la msingi kuzindua mradi wa maji katika eneo hilo.
Akitoa salam na ujumbe wa Viongozi Wakuu wa Serikali, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa wananchi wa wilaya ya Wete , Chongolo ameeleza kuwa;
“Rais Samia ameniambia niwahakikishie kuwa, ataendelea kushirikiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kupambana kwa ajili ya miradi na changamoto zinazowakabili ili ndani ya miaka mitano wilaya ya Wete na Pemba kwa ujumla kuwe na mabadiliko makubwa ya maendeleo.”
Aidha, Chongolo ameeleza kuwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi amemtuma salaam zake kwao, awaeleze wananchi kuwa;
“Anajua changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa baadhi ya maeneo ya Wete, na amewahakikisha maji yatawafikia wananchi wote kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kama ilivyo kwa kijiji cha Taifu kilicho kuwa na uhaba wa maji kwa zaidi ya miKa 14 na sasa maji yanapatikana ya kutosha.”
Aidha katika hatua nyingine Chongolo amewata wananchi wote kuwa macho kupita na kukagua miradi ya ujenzi wa hospitali za wilaya unaoendelea katika wilaya zote za Kaskazini Pemba ikiwemo Wilaya ya Wete ambapo zaidi ya shilingi bilioni 4 zimeshapelekwa na ujenzi unaendelea.
Aidha, Mbunge wa Jimbo Gando Salum Musa Omary ameishukuru chama na serikali kwa kuendelea kushusha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo upatikanaji wa maji katika kijiji cha Taifu ambacho kilikuwa na uhaba kwa zaidi ya miaka 14.
Chongolo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wete inayogharimu shilingi bilioni 4.71 amewataka vijana kuchangamkia fursa za mafunzo ya ufundi na ujuzi zinazotolewa na serikali ili kuweza kujipatia kipato kwa kushiriki ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa na hospitali unaoandela katika maeneo mbalimbali mkoa wa Kaskazini Pemba na Pemba nzima kwa ujumla.
Akizungumza na wanachama na wananchi kwenye kikao cha Mkutano wa Shina Namba 1, Tawi la Kiuyu, Kigongoni, Wilaya ya Wete, ametoa wito kwa wanachama wa CCM wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hiyo mwaka huu, lazima wajipime na wajue wajibu wa uongozi ndani ya chama ndani na nje ya chama, wasisukumwe na tamaa binafsi kutaka uongozi, bali kutumikia watu.
Pamoja na hayo, Chongolo katika maeneo tofuati mkoa wa Kaskazini Pemba amewataka wananchi kuhamasishana na kujiandaa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika mwaka huu, kwani takwimu ni msingi wa mipango ya maendeleo na usambazaji wa huduma za jamii.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mattar Zahoro Mattar amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya CCM, inayoongozwa na Rais Mwinyi imeamua kufanya Pemba kuwa mojawapo ya maeneo ya kimkakati kwa ajili ya uwekezaji kukuza Uchumi wa Buluu, kwa kuwapatia wawekezaji motisha kadri inavyowezekana kujenga mazingira