NA ABDI SULEIMAN.
WANAWAKE wametakiwa kujitokeza kwa wingi, kuomba viwanja vinavyotolewa na serikali na waache kabisa, ile dhana ya kwamba viwanja hivyo hutolewa kwa watu maalumu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Jumuiya ya KUKHAWA Pemba, Hafidhi Abdi Said wakati akifungua mkutano wa kuhamasisha wanawake kumiliki ardhi, uliowashirikishwa wajasiriamali, makundi maalumu na wafanyakazi wa Serikali, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa haki ya umiliki wa ardhi Pemba chini yaufadhili wa FCS na kufanyika mjini Chake Chake.
Alisema katika ugawaji wa viwanja hivyo, serikali haichaguwi wa kumpa ila kinachohitajika ni waombaji kukidhi vigezo vinavyotakiwa.
“Zinapotokea fursa ya kuomba viwanja serikali wanawake mujitokeze kwa wingi kuomba, baadae zinakalia kitako sasa hapo inaweza kuwafirikia, wakitoa 40% basi itakuwa wameshawapita wanaume,”alisema.
Mkurugenzi Hafidhi alisema sasa ni wakati wa wanawake kubadilika katika jamii, ili kuwa na thamani kwa kumiliki mali zao binafsi na sio kuwategemea waume zao tu.
Alisema unapomiliki kiwanja ni chanzo kujikomboa na umasikini, kwani unapomiliki halali unaweza hata kwenda kukopa benk na kupatiwa mkopo husuka unaoutaka.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Zulekha Maulid Kheri, alisema miongoni mwa mambo ya kumuwezesha mwanamke ni kumiliki ardhi kwani ni sehemu ya msingi katika mtaji wa kunyanyua uchumi wake.
Alisema uchumi wowote duniani basi ardhi ni mtaji mkuu, kwani hakuna anaweza kujenga aina yoyote hewani ikiwemo makaazi, viwanda, hata ofisi kubwa za kisasa lazima zitajengwa katika ardhi.
Alisema baada ya kuona hakuna kinachowezekana kufanyika hewani, tumeamua kuwashajihisha wanawake kumilikia ardhi ili ziweze kuwasaidia katika uchumi wao.
“Kila siku tunapiga kelele wanawake wapo chini kimaendeleo, muwezeshe mwanamke sasa ili kufikia malengo yao, tumeona tuanze na hili la elimu kwanza,”alisema.
Kwa upande wao washiriki wa mkutano huo, wamesema upo umuhimu mkubwa wa mwanamke kumiliki kwani ni mkombozi wa maisha yake na jamii kwa ujumla.
Walisema wanapokuwa na shida baada ya kuimiliki halali anaweza kuiyuza, kwa ajili ya kupata fedha na kuwatatulia mataatizo yao makubwa na sio kumtegemea mwanamme.
Walisema ardhi hiyo itaweza kuwasaidia katika shuhuli zake za kiuchumi kwa kupata mikopo mbali mbali katika benk, ili kuendeleza shuhuli zake.