Tuesday, November 26

AMREF yakabidhi vifaa vifaa vya uwezeshaji wa Savailensia ya Magonjwa na matukio yenye athari kiafya.

NA ABDI SULEIMAN.

SHIRIKA la Amref Health Africa Tanzania, kupitia mradi wa Global Health Security Agenda (GHSA)unaofadhiliwa na shirika la Afya la Uthibiti na kuzuia maambukizi ya magonjwa la Marekani (CDC), limekabidhi vifaa vya uwezeshaji wa Savailensia ya Magonjwa na matukio yenye athari kiafya, katika ngazi ya jamii kwenye Wilaya za mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba.

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Shirika Amref Health Africa Tanzania Auganite Musyani, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Afya Salama, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kusaidia utekelezaji utekelezaji wa utoaji wa taarifa ya magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii.

Akitoa taarifa ya utekelezaji ya mradidi wa afya salam Muwakilishi kutoka shirika la Amref alisema mradi umefanikiwa kuzipatia vifaa vya kiutendaji wilaya zote za Pemba kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa taarifa juu ya maradhi mbali mbali katika jamii.

Alisema vifaa hivyo vitasaidia katika kuhakikisha huduma muhimu za afya zinaendelea kutolewa hata katika kipindi cha magonjwa ya mripuko na matukio yote yenye athari kiafya.

Aidha alivijana Vitu ambavyo watavikabidhi kuwa ni pamoja na meza za ofinisi 12, viti vya ofisini 12, printa 4, Komputa 7, UPS 7, Televisheni nne, Komputa ya mkononi moja na vifaa vya kuunganisha na GPS nne.

Hata hivyo aliwataka wasimamizi wa vifaa hivyo kuhakikisha wanavisambaza kwenye vituo vilivyoainishwa na vinatumika nyakazi zote katika utekelezaji wa miradi na shuhuli nyenginezo zenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma wakati wa mripuko.

Mwakilishi huyo wa shirika la Amref, aliwataka wawakilishi wa Madawati ya kusimamia ukusanyaji wa taarifa za mwenendo wa maradhi ya miripuko katika wilaya zote za Pemba ili malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakari, akizungumza kwa niabara ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zakhor Massod, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inashirikiana bega kwa bega na taasisi mbali mbali za kupambana na maradhi ya miripuko, ili kuona malengo ya taasisi hizo yanafikiwa na maradhi ya ondoka nchini.

Aidha alisema ni vyema wawakilishi wa madawati hayo kushajihisha jamii, kutoa taarifa mbali mbali za maradhi ili kufikia lego husika la kupata jamii yenye afya bora.

Alisema afya ya mwanaadamu ni jambo la msingi sana katika ustawi wake, hivyo uwepo wa maarifa ya mtu na upendo yanatokana na kuwa na afya njema.

“Dhamira kuu ni kujenga afya zetu, unaweza kuwa na utajiri wa kutosha ila kama huna afya utajiri unaweza kuukosa, wataalamu wanatuambia mara kwa mara tujaribu kupima afya zetu”

Aidha aliwataka wasimamizi hao kuhakikisha wanavitumia vifaa hivyo, kama dhamira yake inavyoeleza na kuripotia matukio yatakapotokea kama lengo lililokusudia linafikiwa.

Kwa Upande Muwakilishi kutoka shirika la CDC Jeni Kitalile, ameitaka jamii kuyatumia madawati yaliyopo katika wilaya zao kwa kutoa taarifa zinazohusiana na magonjwa mbali mbali, ili ziweze kuchukuliwa hatua stahiki na kwa wakati.

Alisema shirika la CDC limekua likishirikiana kwa karibu na Wizara ya Afya Zanzibar na washirika wao Amref, kwani kumekua na mripuko wa magonjwa na matukio mengine ambayo yamekua yakileta athari za kiafya kwa binaadamu, hivyo CDC limeona kushirikiana na kuanzisha dawati litakalokua linakusanya taarifa kutoka kwa wananchi.

Aliwataka kulitumia hilo dawati kwa kutoa taarifa muhimu zinazohusiana juu ya magonjwa, ili stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Ustawi wa jamii wazee jinsia na watoto Yakoub Mohd Shoka, amewahimiza kuvitumia vifaa hivyo kwa kutoa tarifa husika, pamoja na kuwashukuru Shirika la Amref na CDC, kwa juhudi zao katika Nyanja mbali mbali katika kupunguza athari za ambayo yanaweza kujikinga.

Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Micheweni Hassan Abdallah Rashid, aliwataka wawakilishi wa madawati hayo kuuthamini na kuutunza mchango huo, pamoja na kuwasihi wananchi kutoa taarifa zao sahihi.