(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
KAMBI iliyoanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Kiwani, kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi zilizomo ndani ya jimbo hilo, imeweza kuzaa matunda kwa kutoa Mchipuo na Vipawa Maalumu wanafunzi 20 kati ya 53 walioshiriki kambi hiyo.
Skuli zilizoshiriki katika kambi hiyo ni Kiwani Msingi, Mtangani Msingi, Tasini Msingi, Mwambe Msingi, Minazini Msingi, Mwambe Shamini Msingi.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao 20, Mbunge wa Jimbo hilo Rashid Abdalla Rashid, alisema lengo la kuanzisha kambi hiyo ni kuini viwango vya wanafunzi na kurudisha heshima ya elimu kwenye skuli zilizomo ndani ya jimbo hilo.
Alisema kufaulu kwa wanafunzi 20 ndio waondoshaji wa changamoto za elimu, kwani watahakikisha wanafunzi hao wanafika hadi vyuo vikuu na kurudi kuja kusaidia wenzao.
“Hawa 20 kwa hatua ya awali sio kidogo lengu langu kufikia 100 kwenda vyuo vikuu, wanafunzi mumewaona wenzenu wamefanya vizuri, marahii kambi inaanza mapema lazima tujipange vizuri kuhakikisha tunaweka historia katika jimbo letu,”alisema.
Aidha Mbunge huyo aliwataka wazazi na walimu kushirikiana kusimamia wanafunzi wao, ili lengo la kwenda vyuo vikuu linafikiwa, huku wanafunzi kushuhulikia masomo kwa sasa na sio mambo mengine.
Mapema Kimu Katibu Twala Wilaya ya Mmoani, ambae ni Afisa Mipango wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muumini Abeid, alisema elimu ndio chachu ya maendeleo ya taifa lolote lile, hivyo ipo haja kwa wanafunzi kuzidisha juhudi katika masomo yao.
Alisema Wilaya inamshukuru Mbunge huyo katika jitihada zake za kuongeza ufaulu, huku mikakati ya serikali ni kuongeza vyumba vya kusomea pamoja na skuli za kisasa ikiwemo itakayojengwa Mwambe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mstaafu Issa Juma Ali, aliwataka wananchi kuendelea kuwa na mbunge wao huyo, kwani katika suala la maendeleo kuweka pembeni itikadi za kisiasa ili kufikia maendeleo ya jimbo.
“Niwakati wa kukushuru kwa msaada wako uliouwonesha katika kusaidia wanafunzi, sasa ni zamu ya sisi wanafunzi kuonyesha heshima kwa vitendo,”alisema.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkoani Ali Juma Nassora, aliwataka wabunge wengine kujifunza kutoka katika jimbo la Kiwani, juu ya maendeleo yaliofikiwa na mikakati iyopo,”alisema.
Afisa Elimu Wilaya ya Mkoani Salum Mkuza Sheha, aliwataka walimu kuendelea na kazi yao kwa mwaka 2022 ili kupasisha wanafunzi wengi zaidi.
Akisoma risala katika hafla hiyo Mwenyekiti wa kamati ya Elimu Khamis Ali Khalfan, alisema kambi hiyo imeweza kutoa mchipuo wanafunzi 20 wawili kati yao wamefaulu Vipawa maalumu kati ya wanafunzi 53.
Katika hafla hiyo kila mwanafunzi alipatiwa Pekeji ya Mkoba, ndani mukiwa na Sare, Mabuku mkoba wenyewe na vitu vyengine.