NA ABDI SULEIMAN.
ALIYEKUA kamishana wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan, amesema suala la utunzaji wa amani ya nchi sio kwa vikosi vya vya ulinzi na Usalama Pekee, bali ni jukumu la wananchi wote hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa amani hiyo.
Alisema amani ni tunu, hazina pekee kwa wananchi wa Tanzania na Zanzibar, hivyo mradi wa amani mipakani ni jambo la muhimu katika kuhakikisha nchi inabaki salama muda wote.
Kamisha huyo aliyaeleza hayo wakati akihairisha mafunzo ya siku saba, yaliyoshirikisha makundi mbali mbali, ikiwemo wavuvi, wakulima wa mwani, kamati ya ulinzi na usalama, boda boda, Dereva Tax, watu wa ustawi wa jamii, manahoza, watu wa elimu, walimu wa madrasa, kupitia mradi wa Amani Mipakani unaotekelezwa na CYD kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wete, kwa ufadhili wa Ubalozi wa Canada Tanzania kutipia Mfuko wa Maendeleo ya Kijamii (CFLI).
Alisema Amani Mipakani inahudusha makundi mengi na wananchi wote wanahusika katika ulinzi huo, ikizingatiwa tumezungukwa na bandari bubu nyingi jambo ambalo linapelekea wageni kuingi katika maeneo hayo bila kibali maalumu.
“Ili tuwe na uchumi imara na mzuri, shuhuli za kijamii zieweze kufanyika, itikado za kisiasa ziweze kufanyika tunahitaji kuwa na Amani ya nchini, ikizingatiwa Amani haichaguwi kabila, rangi wala dini,”alisema.
Aidha aliwataka wananchi wa Kisiwa cha Pemba, kuhakikisha wanakua makini na watu wanaingia ndani ya kisiwa hicho kwa kuwafuatilia, kwani kumekua na mtindo wa kuingia kinyume na kufuata taratibu.
Hata hivyo Kamishana huyo alitaka kuhakikisha mafunzo hayo yanafanyiwa kazi na kuwa endelevu kwani bado jamii kubwa inahitaji kupatiwa elimu hiyo.
Mkurugenzi wa CYD Zanzibar Hasimu Ponde alisema lengo la mradi wa Amani Mipakani ni kuongeza ufahamu, uwelewa na kuimarisha ushirikiano kati ya wanajamii pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama katika suala zima la kuangalia mipaka yetu pande za pwani na kuangalia nani anaingia na anafanya nini.
Alisema mradi huo mradi huo umefadhiliwa na balozi wa Canada nchi Tanzania kwa lengo la kuongeza nguvu kwa jamii katika masuala mbali mbali ya ulinzi wa amani.
Naye Katibu Tawala Wilaya ndogo ya Kojani Makame Khamis, alisema mashirikiano ni kitu muhimu kwa wananchi katika kulinda amani ya nchi, hivyo jukumu la kulinda amani sio vikosi vya ulinzi na usalama tu bali wananchi wote.
“Sisi ndio walinzi wa amani na walinzi wakubwa wan chi yetu, tunapokua katika shuhuli zetu mgeni yoyote atakaeingia lazima tuwe na tahadhari nae ili kuepuka kuharibu nchi yetu”alisema.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Afisa Uhamiaji Wilaya ya Wete Haji Omar, alisema idara ya Uhamiaji ndio taasisi pekee yenye mamlaka ya kuruhusu mtu kuingia nchini, baada ya kujiridhisha na vielelezo vyake vyote vinavyohitajika na sio taasisi nyengine.
Naye Mshaidizi Katibu wa Mufti Mkuu Pemba Shekhe Said Ahmad Mohamed, alisema katika kulinda nchi tunawajibu wa kuelimisha jamii, ili kuhakikisha amani na utulivu inapatikana muda wote nchini.