Sadio Mane alifunga mkwaju wa penati ulioiwezesha Senegal kuichapa Misri kwa mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti na kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza, baada ya fainali kumalizika bila bao kufuatia muda wa ziada.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool hapo awali alishuhudia penalti yake ya dakika ya saba ikiokolewa na kipa wa Pharaohs Gabaski.
Mchezaji wa Chelsea Edouard Mendy alimnyima Mohanad Lasheen kumpa Mane nafasi ya kushinda katika uwanja wa Olembe huko Yaounde.
Gabaski alikuwa ameokoa mabao matatu mazuri kutoka kwa Bamba Dieng wa Senegal katika muda wa ziada.
Na katika mechi iliyodaiwa kuwa ni pambano kati ya washambuliaji wa Liverpool, Mane, wa Senegal, na nahodha wa Misri, Mohamed Salah, ni mchezaji wa kwanza Mane aliyekuwa na usemi wa mwisho.
Baada ya kushindwa mara mbili katika fainali za awali, Senegal ndio washindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika hatimaye, huku Misri wakikosa taji la nane la bara ambalo lingezidisha rekodi yao na pia lingekuwa la kwanza kwa Salah.
“Inaonyesha tu kwamba ukifanya kazi kwa bidii, ukivumilia, utapata kile unachotaka,” kocha wa Senegal Aliou Cisse alisema.
“Nina hisia sana kwa sababu watu wa Senegal wametaka kombe hili kwa miaka 60.”
Mechi zote nne za maondoano za Misri kwenye dimba hilo zilienda mbali, na Waafrika Kaskazini walikuwa wamewashinda Ivory Coast na wenyeji Cameroon kwa mikwaju ya penalti kuelekea fainali.
Gabaski alikuwa tayari ameokoa penalti nne kwenye michuano hiyo wakati mechi ilipoenda kwa mikwaju, lakini katika mchuano huo mchezaji huyo wa miaka 33 aliishia kwa kushindwa.
Misri walikuwa wa kwanza kufanya makosa wakati mlinzi wa kati Mohamed Abdelmonem alipoona penalti yake ikigonga upande wa kushoto shemu ya juu ya lango na kutinga mbali – lakini Gabaski alimnyima Bouna Sarr mara moja.
Hata hivyo, Lasheen aliona juhudi zake zikiokolewa na Mane akashinda kwa kumalizia kona ya chini upande wa kushoto.
Mchezaji mwenzake wa Liverpool, Salah hakupata hata nafasi ya kupiga penalti, huku nahodha huyo wa Pharaohs akitarajiwa kushika nafasi ya tano kwa kikosi chake.
Vipigo viwili vya Senegal katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika vilikuja mwaka wa 2002 na 2019.
Na wakati Teranga Lions ikisherehekea hatimaye kushinda michuano hiyo, Misri hivi karibuni watapata nafasi ya kulipiza kisasi, kwa pande hizo mbili kukutana tena mwezi ujao katika mechi ya hatua ya maondoano ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Mane atupa penalti ya mapema
Mechi hiyo ilishuhudia timu ya Senegal iliyocheza bila vizuizi huku Mane akiongoza safu yake ya ushambuliaji dhidi ya safu ya ulinzi ya Misri.
Kikosi hicho kutoka Afrika Magharibi kilipewa nafasi ya mapema ya kuongoza wakati Abdelmonem alipomuangusha beki wa kushoto wa Senegal, Saliou Ciss katika dakika ya nne.
Mane alikuwa na mazungumzo na Gabaski kabla ya kuweka mpira eneo la penalty, akionekana kumwambia kipa huyo arejee kwenye safu yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aligonga mkwaju upande wa kushoto lakini Gabaski alipiga mbizi kwa njia sahihi na kuugonga mpira.
Salah alidhibitiwa vyema na safu ya ulinzi ya Senegal na alikuwa fursa mbili pekee katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilionekena kuvurugika, huku kocha Carlos Quieroz ambaye alikuwa amepigwa marufuku ya kuwa uwanjani, akitaka kuudadali mchezo.
Muda wa ziada ulikuwa wa kusisimua zaidi kwani Senegal walipeleka mchezo kwa wapinzani wao, na Dieng aliona juhudi zake za chini kwa chini zikizuiwa, na mpira mzuri wa kichwa wa chini ukipanguliwa.
Ukombozi kwa Cisse
Senegal imekuwa timu iliyoorodheshwa kuwa bora zaidi barani Afrika kwa miaka mitatu iliyopita chini ya kocha Cisse, ambaye kama mchezaji alikosa penalti muhimu katika mechi ya fainali ya mwaka .
Mane alichangia mafanikio yao makubwa nchini Cameroon, akifunga mabao matatu kwenye michuano hiyo na kuandaa mengine mawili.
Ushawishi wa Salah ulipungua wakati mchuano uliendelea na akaishia kwa timu iliyopoteza kwa mara ya pili kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kuwa sehemu ya timu ya Misri iliyoshindwa na Cameroon mwaka 2017.
Michuano ijayo ya Afcon inatarajiwa kuandaliwa nchini Ivory Coast mwezi Juni na Julai mwakani.
Simba wa Teranga hatimaye walimaliza subira yao ya kunyanyua kombe baada ya uwakishaji wa muda mrefu ambapo nahodha Kalidou Koulibaly akipanda hadi kwenye eneo la watu mashuhuri alipokuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Patrice Motsepe na rais wa Fifa Gianni Infantino kumsalimia rais wa Cameroon Paul Biya.
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI.