Sunday, November 24

Usalama wa rais:Jinsi Marekani inavyotumia msafara wa magari kumlinda rais wake

th

CHANZO CHA PICHA,EPA

Mojawapo ya mambo ambayo watu wengi huwa na hamu ya kujua ni masuala yanayohusiana na ulinzi wa viongozi .

Katika hili Marekani ni mojawapo ya nchi ambazo zimetenga kiasi kikubwa cha fedha katika kumhakikishia ulinzi na usalama rais wake .

Kote anakokwenda rais wa Marekani msafara wake wa magari,ndege na maafisa usalama huwashangaza wengi.

Kimoja kinachojitokeza wazi katika msafara huo kila rais wa Marekani anapokuwa safarini ni wingi wa magari ambayo yanaandamana naye

Lakini kwanini pawe na magari yote haya?

Katika sehemu hii ya kwanza ya makala kuhusu ulinzi wa marais,fahamu mbona msafara huo wa magari unahitajika na jukumu la kila gari katika kumlinda rais wa Marekani

Safari za rais yeyote wa Marekani huwa jambo kubwa lenye mipango kabambe ya kiusalama .

Kwa mfano alipozuru Uingereza mwaka wa 2019 rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliandamana na zaidi ya maafisa 6300 wa usalama na ziara hiyo ya siku tatu iligharimu idara ya Metropolitan Police pauni milioni 3.4.

Ziara yake nyingine mwaka wa 2018 ya siku nne iligharimu zaidi ya pauni milioni 14.2.

Kando na maafisa wa usalama ,vifaa ,magari ,silaha na ndege husafirishwa kwenda anakozuru rais wa nchi hiyo .

Operesheni kama hiyo inahitaji kiasi kikubwa cha raslimali lakini kando na hilo,hebu tuangalie msururu wa magari ambayo kwa kawaida huonekana wakati rais wa Marekani yupo safarini .

Anapokuwa hayupo kwenye ndege yake maalum kwa jina Air Force One ambayo ni ndege ya kijeshi ,rais wa Marekani hutumia usafiri wa gari maalum kwa jina ‘ The Beast’ ambalo wengi wamelisikia au hata kuliona iwe kwenye picha au katika makala yanayozilizungumzia .

Msafara wa rais

Msafara wa rais, unaojumuisha magari mawili ya limousine yanayofanana na magari mengine ya usalama na mawasiliano, husafirishwa mbele ya rais na ndege za usafirishaji za Jeshi la Wanahewa la Marekani wakati anapofanya ziara nje ya nchi ama mbali na ikulu ya Whitehouse

Chini, rais husafiri katika Cadillac One – limousine iliyoboreshwa inayoitwa “The Beast ” kwa sababu zilizo wazi

Gari la ziada, la kupumbaza macho ambalo huambatana nalo lina nambari za leseni za Washington DC – 800-002.

Kizazi cha gari hilo lililotumiwa na Trump kilianza mnamo 2018 – na Secret Service ilituma ujumbe wa Twitter mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba ilikuwa “tayari kuanza kazi ” kabla halijaanza kutumika rasmi .

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Lakini waundaji wa gari hilo General Motors na Secret Service wamesalia kimya kuhusu uwezo maalum wa kiusalama wa gari hilo.

Likiwa na uzito wa takriban tani tisa (lb 20,000) -na mwili uliofunikwa kwa silaha na madirisha ya kuzuia risasi (ambayo hayajafunguliwa yote) – gari hilo linaripotiwa kuwa na uwezo wa kurusha mabomu ya machozi, kamera za kuona usiku na simu ya satelaiti iliyojengewa ndani. .

Matairi yaliyoimarishwa yanazunguka magurudumu ya chuma- ambayo ina maana kwamba gari linaweza kuendeshwa ikiwa matairi hayana hewa

Eneo la abiria linasemekana kufungwa, ili kuzuia shambulio la kemikali, huku vifaa maalum vikizingira tanki la mafuta endapo athari itatokea.

Gari hilo pia lina vifaa vingi vya kielektroniki, Reuters inaripoti.

Linaweza kubeba angalau watu saba na lina vifaa vingi vya matibabu ndani ikiwa ni pamoja na- friji iliyojaa damu inayolingana na aina ya damu ya rais, katika hali ya dharura shirika la NBC linaripoti

Lakini sio hivyo tu.

Wakati rais yuko safarini – utajua .

Magari mengine katika msururu ni magari ya mwanzo na askari wanaotanguliza msafara huo , magari ya maafisa wa Secret service , magari ya kuwabeba maafisa wa kikosi cha kukabiliana na mashambulizi ya hatari, gari la mawasiliano la kivita la SUV, linalojulikana kama Roadrunner, magari ya kuwabeba madaktari na mengine ya kuwabeba waandishi wa habari.

Mpangilio ya msafara wa magari

Mwanzo katika mstari wa mbele kabisa kuna magari ya polisi na pikipiki kwa jina la kiusalama ‘Lead Police’ ambayo kazi yake ni kuondoa chochote barabarani na kutoa tahadhari kwamba msafara wa rais uko nyuma

Kisha kuna gari la rais ‘The Beast’ ambalo huambatana na gari jingine linalofanana nalo

th

Nyuma kuna magari ya maafisa wa Secret Service.

Linalofuata ni gari la wasaidizi wa rais na dakrtari wake kisha kuna gari la ulinzi wa kielektroniki kuzuia mawasiliano yoyote yasiyohitajika .

Nyuma ya gari hilo linafuata gari la kutoa msada na kuthibiti msafara kwa jina ‘Control and Support’.

Linafuata gari la kikosi maalum cha kujibu shambulizi ambalo nyuma yake kuna gari la kikosi cha kukusanya habari za kijasusi .

Linafuata gari maalum la kushughulikia kemikali au vifaa hatari kisha nyuma yake kuna magari yanayowabeba waandishi wa habari.

Nyuma ya wanahabari kuna kikosi maalum cha mawasiliano ya setalaiti kinachofuatwa na ambulansi .

Wanaofunga msafara ni maafisa wa usalama kwenye magari ya ziada na pikipiki mbao huitwa ‘Rear guard’.

CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI.