NA ABDI SULEIMAN.
WANAFUNZI wa Skuli ya Kinyasingi Sekondari na Istaqama Sekondari Wilaya ya Wete, wameitaka Jumuiya ya kuwezesha vipaji vya Vijana Pemba(YETA), kufika vijijini kutoa elimu juu ya udhalilishaji na migogoro, kipindi cha mavuno ya zao la karafuu ili kuwanusuru na vijana ambao hawako skuli.
Wakitoa maoni yao kwa nyakati tafauti, katika mikutano iliyoandaliwa na jumuiya ya YETA kupitia mardi wa kujenga uwelewa kwa vijana, katika kuzuwia ukatili na migogoro katika kipindi cha mavuno ya zao la karafuu Pemba.
Wanafunzi hao wamesema vijana waliowengi ambao hushiriki katika zoezi hilo la uwokotaji wa mpeta, wako mitaani hivyo iwapo elimu hiyo iytaweza kuwafikia basi yataweza kuondokana na tabia hiyo.
Amora Khamis Juma kutoka Skuli ya Kinyasini Sekondari, alisema matukio ya udhalilishaji hutokea muda mwingi katika kipindi cha mavuno ya karafuu.
“Utamkuta mtoto anarudi kuchuma karafuu na kichi 5 au 6 au nne za karafuu mbichi, jee kuna mpeta gani huo mtu anayeweza kupata karafuu kiasi hiko,”alisema.
Yusra Juma Khalfan kutoka Skuli ya Istaiqama Sekondari, alisema kipindi cha mavuno ya karafuu hata suala la masomo kwa wanafu hupungua, hali inayopelekea migogo baadhi yao kuonana wabaya pale wanapowatakataza.
Aidha aliitaka YETA, kuhakikisha inakua mstari wa mbele kawenye kutoa elimu juu ya suala la migogoro kwa wakulima wa karafuu ili kutokuchukua hukumu mikononi kwao.
Naye Yussuf Juma Salim, aliwataka wanafunzi wenzake kuacha kujihusisha katika mambo ambayo yatapelekea kukatisha ndoto zao katika suala zima la elimu.
Akiwasili mada kwa wanafunzi katika kuzuwia masuala ya udhalilishaji na migogoro, kipindi cha mavuno ya zao la karafuu Mwezeshaji Sada Aboubakar Khamis, alisema baadhi ya wanawake hujenga ukaribu na mchumaji wa karafuu, kwa lengo la kukatia vitawi au kupatia katafuu kidogo.
“panapotokea masuala ya ubakaji kunapelekea kuongokeza kwa watoto wa mitaanii baada ya tendo la udhalilishaji kufanyika, wakati wote hawana uwezo wa kutunza mtoto na kesi hizi zipo na zimeshatokea katika mpeta wa karafuu”alisema.
Naye Dk.Ali Yussuf Ali ambaye ni mwezeshaji, alisema kipindi cha Karafuu Mogogoro mingi hutokea katika jamii na kusababisha uvunjifu wa amani, jambo ambalo linapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
“Hakuna atakae kupa karafuu bure au zawadi, lazima huyo atakuna na yeye anakitu anategemea, tunapaswa kujifunza kukataa au hapa ikiwa mtu humfahamu”alisema.
Hata hivyo alisema uchumaji wa karafuu bila ya vitendo vya udhalilishaji au kutokea kwa migogoro unawezekana, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini.
Mapema mjumbe wa Jumuiya ya YETA Pemba Haroub Ali Nassor, alisema vijana wanaushawishi mkubwa katika jamii, hivyo wameamua kuwatumia wanafunzi kwa lengo la kufikisha ujumbe huo kwa wenzao.