Watendaji wa Wakala wa chakula ,Dawa na Vipodozi wakiteremsha bidhaa ya tende iliyopita muda wa matumizi kwa ajili ya uteketezaji katika jaa kuu la Kibele Zanzibar.
Watendaji wa Wakala wa chakula ,Dawa na Vipodozi wakiteremsha bidhaa ya tende iliyopita muda wa matumizi kwa ajili ya uteketezaji katika jaa kuu la Kibele Zanzibar.
Mkaguzi Mkuu wa chakula na utekelezaji , wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi ZFDA Sleiman Akida Ramadhan akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kukamilika zoezi la uteketezaji wa tani 29 za bidhaa ya tende iliyopitwa na muda ambayo ilikamatwa katika ghala lisilorasmi linalomilikiwa na Bwana Hafidh Salim Ali Kilimahewa Zanzibar .
Afisa Mazingira kutoka mamlaka ya usimamizi wa Mazingira Laylat Mussa akitoa ufafanuzi juu ya athari za kimazingira zitokanazo na uteketezaji wa bidhaa zilizopitwa na muda mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uteketezaji wa tende uliyofanyika jaa kuu la kibele Zanzibar.
Bidhaa ya tende iliyopitwa na muda ikiwa imehifadhiwa katika ghala lisilorasmi huko Kilimahewa Wilaya ya Mjini Unguja kabla ya zoezi la uteketezaji .
Bidhaa ya tende iliyopitwa na muda ikiwa imehifadhiwa katika ghala lisilorasmi huko Kilimahewa Wilaya ya Mjini Unguja kabla ya zoezi la uteketezaji .
PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Bodi ya chakula dawa na vipodozi ZFDA imesema jumla ya tani 29 za tende ya kula iliyomalizika muda wake imeteketezwa huko katika jaa la Kibele Unguja.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uteketezaji wa bidha hiyo Mkaguzi Mkuu wa Chakula na utekelezaji Suleiman Akida Ramadhani amesema tende hizo zilizomaliza muda wake zimegundulika huko katika ghala bubu ilioko Kilimahewa na kujulikana na wasamaria wema.
Pia amesema wananchi waligundua kwa kusikia harufu na nyengine kutupwa mitaani katika sehemu za Welezo na haraka kupeleka taarifa kunakohusika na kuchukuliwa hatua za haraka.
Amesema iko haja ya kutolewa elimu kwa wafanyabiashara wanaoleta bidhaa zilizokuwa zimeshamaliza muda wake kuacha tabia hiyo kwani inaweza kuathiri jamii kwa kutumia bidhaa hizo.
Aidha amesema bidhaa hiyo itakapotumika itaweza kuathiri afya ya mlaji kwa kemletea madhara makubwa athari hizo ni pamoja kupata madhara ndani ya mwili .
Pia amesema mfanyabiashara aliyehusika na bidhaa hiyo ni Hafidh Salim Ali na kulipia gharama zote za utekelezaji huo.
Nae Afisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mambo ya hali ya hewa Lailati Mussa Foum amesema bidhaa zilizoharibika zinahitaji kuteketezwa kwa haraka kwani sio sahihi kutumika kwa jamii.
Hivyo amesema wafanyabiashara wahakikishe wanaoleta bidhaa zilizokuwa salama kwa matumizi, ziwe na viwango na iwapo zitagundulika kubakia muda mdogo kumalizika zisiingizwe nchini kwani hazitoruhusiwa .
Kwa upande wa wananchi wameishukuru Bodi ya chakula ,dawa na vipodozi kwa kuchukua hatua za haraka kuteketezwa bidhaa hiyo hasa ukizingatia mwezi mtukufu wa Ramadhani unakaribia na kuogopa isije ikatumika.