Saturday, March 15

VIDEO: Wanafunzi kutoka skuli nne za Pemba wanufaika na miradi ya milele wazawadiwa.

Na Raya Ahmada.

Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation imesema itaendelea kuekeza vijana katika suala la elimu kwa kuwajenga kuwa wabunifu ili wawezekuingia katika ulimwengu wa kazi.

Kauli hiyo imetolewa Baraza la Mji Chake Chake na Mkuu wa Miradi ya Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Khadija Ahmed Sharif kwenye sherehe za kuwazawadia wanafunzi waliopasi michipuo na vipawa wa darasa la sita kutoka skuli ya Mnarani, Michenzani, Pujini na Sizini na kukabidhi shilingi laki 8 kwa skuli ya mnarani iliyofanya vizuri zaidi.

Amesema hatua hiyo itawasaidia vijana kuwa na mwamko wa kupata kitaaluma na fani mbali mbali ambazo zitaweza kutatua change moto ya upatikanaji wa ajira.

Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Abdalla Said Abdall amesema tokea taasisi hiyo kuwekeza katika elimu imeleta mabadiliko makubwa ya ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao ya taifa.

Akitowa nasaha zake kaimu Afisa Mdhamini wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Suleiman Hamad Suleiman ameipongeza taasisi ya milele na kuwataka wanafunzi hao kuongeza juhudi katika masomoyao ili wafanye vizuri katika mitihani yao.

Akitowa neno la shukrani mwalimu Ali Massoud Ali kutoka skuli  ya mnarani na Abdal-rahman kutoka Fidel Castro wamesema.

 

KUANGALIA VIDEO YA HABARI HII BOFYA HAPO CHINI.