NA ABDI SULEIMAN
TAASISI ya Milele Zanzibar Foundation imesema kuwa itaendelea kuekeza kwa vijana katika suala la elimu kwa kuwajenga kuwa wabunifu ili waweze kuingia katika ulimwengu wa kazi.
Milele imesema kuwa ikiwa vijana watajenga ipasavyo kuwa wabunifu katika fani mbali mbali, basi wataweza kushindana na kuibuka washindi kupitia fani zao walizojengwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Miradi kutoka Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Khadija Ahemed Shariff, katika hafla ya kuwazawadia wanafunzi 64 waliofauli sita waliofaulu mchipuo na Viwapa, kutoka skuli zilizofanya vizuri zilizomo katika shehia zilizomo katika miradi ya milele.
Aidha alizitaja skuli hizo kuwa michezani msingi, sizini msingi, Pujini Msingi na Skuli ya Mnarani Makangale ambayo imeweza kupasisha wanafunzi zaidi ya 20 mwaka huu.
Aliwashukuru walimu wa skuli hizo kwa kazi kubwa walioifanya katika kuwasaidia wanafunzi na kuweza kutimiza ndoto zao za kimasomo kwa kufauli katika hatua ya kwanza.
“Matokeo ya STD 2021 yamewafanya kuhamasika zaidi na kuona wananfunzi wa skuli hizo wanawatunza, ili skuli zilizobakia nazo zifanye vizuri zaidi, hizi ni zile wanafunzi kuanzia 10 kwenda mbele ndio tuliowatunza, mwakani mategemeo skuli zote 22 zinapasisha na tutawatunza”alisema.
Hata hivyo mkuu huyo wa miradi, aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pembakuwasaidia walimu wanaosomesha skuli zilizoko vijijini kwa kuwapa motisha maalumu, iliwaweze kufanya vizuri kazi zao kwani walimu hao wamekua na mchango mkubwa kwa skuli hizo.
Mapema mgeni Rasmi katika hafla hiyo, kwaniaba ya Afisa Mdhamini WEMA afisa Elimu ya Sekondari Suleiman Hamada Omar, alisema hakuna kitu cha kuekeza kwa watoto kama suala la elimu, hivyo kujitahidi kuendeleza kusoma kwa bidii.
Aidha liwashukuru wanafunzi waliofaulu masomo yao, huku akiwataka kuendelea na kasi hiyohiyo na sio kurudi nyuma badala yake wafanye vizuri katika masomo yaliyoko mbele yao na kufikia hadi vyuo vikuu.
“Leo hapa kila mtu anafuraha musije mukageuka mgema baada ya kusifiwa tembo akalitia maji, kazi kubwa bado iko mbele yenu kila mmoja anamalengo yake jitahidini kufikia malengo hayo”alisema.
Naye mwakilishi kutoka Fatma Issa Foundation Hadia Othaman, “Kipindi kifupi nipo Pemba ila nimegundua watoto wahuku wanaakili sana na hata kama watashindana na wanafunzi kutoka Marekani basi mwanafunzi wa Pemba ataweza kushinda tu, hili ni jambo la kujivunia na nimafanikio makubwa haya”.
Mratib wa Milele Zanzibar Foundation Ofisi ya Pemba Abdalla Said Abdalla,alisema Taasisi ya Milele inafanya kazi katika miradi mbali mbali, ikiwemo Elimu, Afya, Miundombinu, Maji na Pemba imo katika shehia 24.