
CHANZO CHA PICHA,RICARDO SENRA/TWITTER
Picha ya fenesi linalouzwa moja kwa pauni 160 au dola 218 huko Uingereza imezua gumzo sana mitandaoni .
Picha hiyo ilipigwa na ripota wa BBC Ricardo Senra na kusambaa kwenye mtandao wa Twitter akiwa katika nchi yake ya Brazil, na watu zaidi 100,000 walitoa maoni yao: Fenesi linauzwa kwa pauni 160, takriban $218, katika Soko la Borough, mojawapo ya soko kuu la chakula London.
Bei hiyo ya juu imewashtua baadhi ya watumiaji wa Twitter. Wengi walitania kwamba wangesafiri kwa ndege hadi Uingereza ili kuwa “mabilionea” kwa kuuza tunda hilo.
Baada ya yote fenesi safi linaweza kupatikana katika maeneo mengi ya Brazil kwa $ 1.10 kila moja, na inaweza kununuliwa sawa katika nchi nyingine nyingi za kitropiki.
Kwa hivyo ni nini kinachoelezea bei hiyo ya juu kwa tunda moja, ambalo linachukuliwa kuwa “la kigeni” na watumiaji wengine? Na kwa nini mahitaji ya kimataifa yameongezeka hivi karibuni?
Kwanza kabisa, ni muhimu kukumbuka kanuni ya msingi: hatua ya kuuza inaathiri bei na hii inatumika kwa bidhaa yoyote.
“Hata nchini Brazil, bei ya fenesi inatofautiana. Kuna mahali ambapo inawezekana kuchuma kutoka kwenye mti bila malipo. Katika sehemu nyingine, ni ghali sana,” Sabrina Sartori, mkurugenzi mkuu wa Estancia das Frutas, bustani ambayo ni makao kwa aina 3,000 za matunda katika jimbo la Sao Paulo.
Pia, fenesi haziwezi kulimwa kwa ajili ya biashara katika nchi baridi zaidi, kama vile Uingereza.
Lakini kuna zaidi ya hayo. Biashara ya kimataifa ya fenesi ni ngumu sana na hatari, wanasema wataalam, kwa sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na asili yake ya kuharibika, msimu na kiasi.
“Fenesi ni nzito sana, hukomaa haraka sana na ina harufu ya kipekee ambayo haipendezi kwa kila mtu,” anaongeza Sartori.
Uzito wa hadi 40kg, matunda, asili ya Asia, yanaharibika sana na hayadumu kwa muda mrefu sokoni.
Mbadala kwa wasiokula nyama
Mara nyingi tunda hilo haliwapendezi watu katika nchi ambapo hukuzwa na fenesi limeanza kuvutia wengi wanaolitaka katika mataifa yaliyoendelea yanayoendeshwa na walaji mboga ambao kamwe hawali nyama , ambao huona kama mbadala wa nyama.
Linapopikwa, umbile lake hufanana na nyama ya ng’ombe au nguruwe, na kulifanya kuwa mbadala maarufu isiyo na nyama kama vile tofu isiyo na gluteni.
Nchini Uingereza pekee, idadi inayoongezeka ya walaji mboga pekee inakadiriwa kuwa milioni 3.5.
Hata hivyo, wakati fenesi linakuwa limeiva, na mchakato huu hutokea kwa haraka sana, linachukua ladha tamu na linaweza kutumika baada ya mlo.
Njia mbadala ya bei nafuu zaidi kwa watumiaji, kwa hiyo, ni kununua ikiwa kwenye mikebe.
Fenesi iliyopakiwa kwenye mikebe inaweza kupatikana katika maduka makubwa ya Uingereza kwa karibu $4 kwa wastani, lakini wengi wanasema haina ladha sawa.
Ukubwa wa fenesi
Fenesi pia ni kubwa sana, ambalo linafanya kuwa vigumu kusafirisha na mavuno yake ni ya msimu. Upakiaji ni changamoto kwa sababu ya umbo na uzito.
Haliwezi kuwekwa kwenye masanduku ya ukubwa wa kawaida kama matunda mengine.
Pia hakuna njia ya kisayansi ya kujua ikiwa tunda liko katika hali nzuri kwa kuangalia nje .
Kwa kuongezea, katika nchi zinazokuza tunda hili na kuuza nje, haswa Kusini na Kusini-mashariki mwa Asia (Fenesi ni tunda la kitaifa la Bangladesh na Sri Lanka), msururu wa uuzaji haupo na mazoea ya taratibu za baada ya mavuno hazipo.
Kwa hivyo , inakadiriwa kuwa 70% ya uzalishaji wote hupotea.
Nchini India, kwa mfano, fenesi linachukuliwa kuwa tunda lisilofaa na linanyanyapaliwa katika maeneo ya vijijini kama tunda la maskini.
Cha ziada, wataalam wanasema, ni ukosefu wa ujuzi: Ingawa fenesi limekuwa maarufu zaidi, watumiaji wengi hawajawahi kujaribu na hawajui mapishi yoyote ambayo yanaweza kufanywa nalo.
Uagizaji
Fabricio Torres, mmiliki wa Torres Tropical BV, muagizaji wa matunda ya kigeni nchini Uholanzi, anasema kwamba shehena zinazoagizwa kwa ndege zimeongezeka sana kutokana na janga la covid-19.
“Matunda mengi kutoka maeneo ya Asia na Amerika Kusini hufika Ulaya kwa ndege za abiria. Mashirika ya ndege sasa yanatafuta bidhaa za ongezeko la thamani kwa nafasi ya mizigo.
Fenesi huharibika haraka sana , kwa hiyo haifai kuagizwa kwa kiasi kikubwa. Haya yote yanaongeza bei ya mwisho,” anafafanua.
Licha ya vizuizi vyote, tafiti za hivi karibuni zinakadiria upanuzi wa soko la kimataifa la fenesi
Kulingana na makadirio kutoka kwa kampuni ya ushauri ya IndustryARC, inatarajiwa kufikia dola milioni 359.1 ifikapo 2026, ikikua kwa kiwango cha kila mwaka cha 3.3% katika kipindi cha 2021-2026.
Mnamo 2020, eneo la Asia-Pasifiki lilichangia sehemu kubwa zaidi ya soko la fenesi (37%), likifuatiwa na Uropa (23%), Amerika Kaskazini (20%), ulimwengu wote (12%), na Amerika Kusini. (8%). , uthibitisho zaidi kwamba Waamerika Kusini, hasa Wabrazili, wana fenesi zao
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI.