Friday, November 15

Ofisi ya mufti wakutana na walimu wa madrasa za dufu Kisiwani Pemba.

NA ABDI SULEIMAN.

OFISI ya Mujfti Mkuu wa Zanzibar, imewataka walimu wa madrasa za dufu Kisiwani Pemba, kutochaganganyika kwa wanawake na wanaume katika shuli zao za upigaji wa dufu, kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi na maadili ya kiislamu.

Kauli hiyo imetolewa na katibu Mtendaji Ofisi Mufti Zanzibar Shekh Khalid Ali Mfaume, wakati alipokua akizungumza na waalimu wa madrasa Pemba Mjini Chake Chake.

Alisema upigaji wa dufu wa sasa umekua ukienda kinyume na maadili ya dini ya Kiislamu, kutokana na kuchanganyika kwa wapingaji wake jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo hapo baadae.

“Pamoja na upigaji wa Dufu kumeonekana kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili, sisi tuliopewa nafasi hatuwezi kutizama haya ni kuona upigaji wa madufu unakiuka maadili ya dini”alisema.

Alifahamisha upigaji wa dufu ni kinyume na utaratibu na sheria ya dini ni, kuwepo mchanganyiko baina ya wanawake na wanaume, huku wanawake wakichezesha miili yao mbele ya wanaume kitu kinachofanyika hivi sasa.

Aidha alisema haiwezekani kuchukuliwa nyimbo za bongo fleva na tarabu, kuzipeleka katika dini hiyo ni kuharibika kwa maadili wakati watu wanaweza kuiyondosha.

Hata hivyo alisikitisha na kutumika kwa aya za Quran katika upigaji wa dufu huku wanawake wakicheza, huku akisikitishwa na baadhi ya wanawak ekucheza na miili yao kuitoa katika madirisha ya gari.

Wakichangia katika kikao hicho, baadhi ya walimu wa madrasa za dufu Pemba, wameishauri ofisi ya Mufti kuvichgukulia hatua vyuo vinavyokwenda kinyume na maadili.

Mwalimu Said Bakar Hamad kutoka Mbuzini, aliitaka aofisi ya Mufti kutambua kuwa hilo jambo halikuanza sasa bali lilianza zamani, hivyo aliwataka walimu wenzake kulinda maadili ya dini, pamoja na kurudisha utamaduni wa zamani ya maulidi ya dugfu na minanda.

“Ofisi ya Mufti inapaswa kutoa tamko kuwa wanataka Qaswida hii na Mnanda huu, chengine chochote kitakachopigwa basi hatua kali zichukuliwe kwa wahusika”alisema.

 

Naye Hafidh Abdi Bakar alisema, ofisi ya mufti mpaka sasa ipo juu ya mstari kutokana na hali hiyo iliyojitokeza, huku akiwataka kutokuonea haya au upendeleo wa chuo chochote kitakacho husika katika kipindi hiki.

“mimi madrasa yangu ni mwaka wa 25 sijawahi kuona ukaguzi wowote kutoka ofisi ya mufti kuja kufanya ukaguzi, hili ni tatizo linallopelekea yote,”alisema.

Baadhi ya Viongozi wa Vyuo hivyo wamitaka ofisi ya Mufti Pemba, kupitia na kuhakiki vyuo vyote, ili kubaini vyuo vinavyolenga kuharibu uislamu.

MWISHO