NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Wananchi katika Shehiya ya Gombani Wilaya ya Chake Chake wametakiwa kuwa tayari kutoa mashirikiano yao katika kazi Utambuzi wa ardhi pindi itakapoanza kazi hio ili iweze kufanikiwa kama ilivyopangwa.
Akizungumza na wadau wa utambuzi wa ardhi katika shehi ya ya Gombani katika mkutano wa siku moja huko katika ukumbi wa Tassaf Chake Chake Mkuu wa Wilaya hio Abdalla Rashid Ali amesema hio ni fursa muhimu kwa wakaazi wa maeneo hayo kwani baada ya kazi hio kila mmoja ataweza kufahamu eneo lake.
Kwa pande wake AfisaMdhamini Wizara ya ardhi maendeleo ya makaazi Bakar Ali Bakar amesema hivi sasa kuna wimbi kubwa la migogoro ya ardhi hivyo kupitia kazi hio ana imani matatizo hayo yataondoka au kupungua kwa kiasi kikubwa.
Akielezea lengo la utambuzi huo mkuu wa upimaji na ramani Salim Khamis Haji amesema baada ya utambuzi kila mmoja atapata kufahamu mipaka yake lakini pia ataweza kupata hati ya umiliki kihalali ardhi hio
Nao wananchi hao wamesema katika kutekeleza kazi hio ni vyema kuzingatia mipango ya miji kwani mji wa Gombani kwa sasa unatoa sura mya kwa kisiwa cha Pemba.
ANGALIA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPO CHINI