Friday, November 15

HABARI PICHA: Kamisheni ya Ardhi watoa elimu ya usajili wa ardhi na utatuzi wa migogoro kwa wananchi wa wilaya ya Wete.

WASHIRIKI wa Kikao cha kujadili masuala ya ardhi na utatauzi wa migogoro, kilicho washirikisha masheha, wananchi na watendaji wa serikali na kufanyika jamhuri holi Wete
NAIBU Mrajis wa Ardhi Pemba Asha Suleiman Said, akiwasilisha mada sheria na taratibu za ardhi katika utatuzi wa migogoro, kwa masheha wananchi na watendaji wa serikali mkutano uliofanyika Jamhuri Holi Wete
MKUU wa Wilaya ya Wete Hamadi Omar Bakar, akizungumza na msheha, wananchi na watendaji wa serikali Wete, katika kikao cha kujadilia kuhusu Masuala ya Ardhi na utatuzi wa migogoro, kikao kilichofanyika Jamhuri holi Wete.
IPO haja kwa taasisi husika kutoa elimu ipasavyo juu ya uwanikaji bora wa biashara ya Dagaa, pichani waanikaji wakianika chini kwenye nyavu huko bandarini Tumbe Wilaya ya Micheweni
WAVUVI wa Samaki katika bandari ya Mkoani, wakiwa na samaki wao baada ya kurudi kuvua na kusubiri kuwapeleka mnadani kwa ajili ya kuwauza, kama wanavyoonekana katika picha

(PICHA NA ABDI SULEIMAN)