Thursday, January 9

WAZIRI HAROUN AKABIDHI MISAHAFU 200 KWA MASJID MUNAUWAR

NA ABDI SULEIMAN.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman, amekabidhi Misahafu 200 kwa uongozi wa Masjidi Munauwari Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwaka wakati wa ufunguzi wa msikiti huo.

Waziri huyo alisema amesema misahafu hiyo itaweza kuwasaidia waumini wa mskiti huo, pamoja na wanafunzi wanosoma katika madrasa iliyopo msikini hapo.

Akikabidhi misahafu hiyo kwa niaba ya Waziri Haroun, msaidizi Katibu wa Mufti Pemba Sheikh Said Ahmad Mohamed, alisema utekelezaji wa msaada huo ni kuonesha mfano mzuri kwa jamii ikiwemo kutimiza ahadi hiyo.

“siku ya ufunguzi wa msikiti wetu huu, Waziri Haroun aliahidi kusaidia misahafu na leo ameweza kutimiza ahadi yake kwa vitendo”alisema.

Aidha shekhe Said aliwataka viongozi hao kuifahamisha jamii kwamba, ahadi iliyowekwa imetimizwa na kwa vitendo na kuwataka itumike kwa lengo lililokusudiwa.

Akipokea misahafu hiyo kwa niaba ya wananjamii na kamati ya masjid Munauwar Mfikiwa, kaimu imamu wa msikit huo Khamis Mkadi, alisema msaada huo wameupokea kwa moyo mkunjufu na kuahidi kuwa misahafu hiyo itatumika kwa lengo lililokusudiwa.

Alisema misahafu 200 ni mingi kama haitotumika ipasavyo, lakini sio mingi ikiwa itafanyiwa kazi, hivyo misahafu hiyo itaweza kugaiwa hata katika madrasa iliyopo msikitini hapo.

“hii nimiongoni mwa sadaka zenye kuendelea kwa mtoaji, tunamshukuru Waziri Haroun kwa kutekeleza na msfikishie salamu zetu kama tumepokea na tunamshukuru”alisema.

Aidha kaimu imamu huyo alitumia nafasi hiyo, kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu, viongozi wa Taifa wa Zanzibar ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kulinda na kutunza maendeleo yanayotolewa.

MWISHO