Saturday, March 15

HABARI KATIKA PICHA: msafara wa vijana wa kuhamaisha amani na mtengamano wa jamii, kupitia mradi wa mtengamano wa jamii na amani Zanzibar,ulivyofika kisiwani Makoongwe

AFISA Uchechemuzi na Mawasiliano kutoka taasisi ya Norwegian Church Aid Tanzania Nizar Seleman, akitoa taarifa fupi ya msafara wa vijana wa kuhamaisha amani na mtengamano wa jamii, kupitia mradi wa mtengamano wa jamii na amani Zanzibar, kwa wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Wilaya ya Mkoani, mradi huo ukiwa na kauli mbiu ‘’ Amani Yetu, Kesho Yangu’’.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MUWAKILISHI kutoka taasisi za kidini zinazoshirikiana katika kutunza amani Zanzibar (ZANZIC) Profesa Issa Haji Zidi, akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Makoongwe wakati wa msafara wa vijana wa kuhamaisha amani na mtengamano wa jamii, kupitia mradi wa mtengamano wa jamii na amani Zanzibar, kwa wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Wilaya ya Mkoani, mradi huo ukiwa na kauli mbiu ‘’ Amani Yetu, Kesho Yangu’’.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)