Thursday, January 16

WANANCHI WASHAURI KUKATA TIKETI KATIKA VITUO HUSIKA NA SIO MIKONONI KWA WALANGUZI

 

NA ABDI SULEIMAN.

ABIRIA wanaosafiri na meli kupitia bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba, wameshaurikia kukata tiketi katika vituo halali vya mawakala wa meli na sio kununua tiketi kwa walanguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari hizi, mara baada ya kukamilizika kwa zoezi la ukaguzi wa tiketi za abiria, utaratibu wa utoaji wa magari ya miziko bandarini na taratibu za meli kuondoka katika bandari ya Mkoani.

Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasialiano na Usafirishaji Pemba Ibrahim Saleh Juma, alisema zoezi hilo litakua endeleo kwa kuhakikisha abiria anakata tiketi kwa kutumia kitambulishio Chake.

Alisema haipendezi kuona abiria anatumia walanguzi katika kununua tiketi, wakati vituo halali vipo hivyo anapaswa kufahamu kuwa hatiosafiri kwa tiketi hiyo.

“Tunachotaka kuona kila abiria anasafiri kwa kufuata taratibu na kanuni za bandari wakati wote anapokua safarini, kwenda kinyume kutapelekea kutokusafiri kwake”alisema.

Akizunguzmia suala la mizigo, Mdhamini Ibrahim alivitaka vitengo vinavyohusika na mapato bandarini hapo kuhakikisha vinakua makini na ukusanyaji wao, kwa kutokuruhusu gari na mizigo kupita bila ya kulipia urushuru.

Naye kaimu Mkurugenzi ulinzi na usalama shirika la bandari Zanzibar Omar Khamis Ali, aliwataka wananchi kufuata utaratibu na sheria za bandarini, wakati wote wanapotaka kusafiri au kupokea wageni wao.

Alisema isipofuatwa sheria na taratibu amani na utulivu iliyopo inaweza kupotea, hivyo wanapaswa kuhakikisha wanailinda na kuitunza amani hiyo, kwa kufuata na kutekeleza kwa vitendo taratibu zote.

“Ziara yetu hii ni miongoni mwa taratibu zetu za kazi, kuhakikisha abiria wanaosafiri wanasafiri salama na kufuata taratibu na sheria”alisema.

Akizungumzia Changamoto zilizojitokeza, alisema ni ufanyaji kazi kimazowea kwa watendaji, hali inayopelekea kutokufuata taratibu na sheria kwa wafanyakazi wa bandarini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi huduma za Meli na Bandari, kutoka Mamkla ya Usafiri baharini Zanzibar (ZMA) Rajab Ali Rajab, alisema operesheni hiyo ni utaratibu wa kawaida kwao, katika kuona sheria na taratibu zote zainafuatwa.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vyao halali pamoja na tiketi wakati wote wanapohitaji kusafiri ikiwa wanaenda Unguja au anatoka unguja kuja Pemba.

MWISHO