Thursday, November 14

KAMISHENI YA ARDHI YAKUTANA NA MASHEHA WIYALA YA WETE

NA ABDI SULEIMA.

MASHEHA Wilaya ya Weye Mkoa wa Kaskazini Pemba, wamewashauri wananchi kfuata sheria na taratibu wakati wanapotaka kuuziana ardhi au kurithishana, ili kupunguza migogoro isiyo kuwa ya lazima.

Wamesema kuwa kumekua kukijitokeza migogoro mingi ya ardhi katika jamii, unapofuatilia inatokana na sheria kupindishwa wakati wa mauziano au urithishaji wake.

Masheha waliyaeleza hayo wakati walipokua wakizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumalika kwa kikao cha kujadili masuala ya ardhi na utatauzi wa migogoro, huko Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Sheha wa shehia ya Kipangani Makame Seif Faki, alisema licha ya elimu kutolewa kwa jamii, bado migogoro ya ardhi imekua ikijitokeza kidogo kidogo, kufuatia sheria kutokufuatwa wakati wa kuuziana kwa mali.

“Kwa sasa migogoro inayojitokeza ni migo migodo, kamisheni ya ardhi inajitahidi kutoa elimu kwa wananchi, kuweza kusajili ardhi zao na kutambuliwa kabisa, unapofanya hivyo basi ardhi hiyo inakua halali kwako”alisema.

Naye sheha wa shehia ya Limbani Massoud Ali Hassan, aliyomba serikali kuendelea na masuala ya utambuzi wa ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi kwa jamii.

Alisema ardhi inayotambuliwa na kusajiliwa inakua ardhi halali kwa matumizi yoyote yale, tafauti na ardhi ambayo haijatambulika haishi migogoro.

“Unaposajili ardhi yako kisheria basi ardhi hiyo inakua salama zaidi, serikali pia inaitambua na unaweza hata kufanya miamala mbali mbali ya mabenk kwa kutumia ardhi hiyo”alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanafuata taratibu wakati wanapouziana ardhi au kufanya mirathi kisheria, ili kuepusha kuzulumiana na kutokea kwa migogoro.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakar, alisema migogoro mingi inayojitokeza inatokana na changamoto nyingi ni ardhi, asilimia 70 hadi 80 ni migogoro ya ardhi.

Alisema bado jamii hususan vijijini inahitaji kupatiwa elimu ya uwelewa juu ya utambuzi wa ardhi, ili kuepuka migogoro ya ardhi kwani jamii iliyokubwa imekosa uwelewa huo.

Hata hivyo alisema uwelewa ukiwepo hata nguvu za migogoro inaweza kupunguza moja kwa moja katika jamii, hivyo kamisheni inapaswa kuendelea kutoa elimu kwa jamii.

“elimu hii ni muhimu kwa wananchi tena vijijini kutolewa, washiriki elimu hii kama mutaitumia ipasavyo basi jamii iliyokubwa itaweza kuelimika sana”alisema.

Mapema afisa usajili wa ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo, alisema lengo la kikao hicho ni kupunguza kabisa migogoro ya ardhi, kwani migogoro mingi imekuwa ikizuka kwa wananchi kuvamia maeneo mbali mbali.

Aliwataka wananchi ambao wameshatambuliwa katika wilaya ya wete, kufika kamisheni ya ardhi kuchukua hati zao za umiliki wa ardhi ikiwemo shehia ya limbani, kiungoni na Selemu.

Kwa upande wake Naibu Mrajis wa Ardhi Asha Suleiman Said, aliwashauri wananchi kuhakikisha migogoro ya ardhi inapotokea sio kukimbilia katika vyombo vya sheria, jambo ambalo litapelekea kuongezeka kwa uhasama wakati wanapaswa kukutana kwa hatua za awali kusuluhishana wenyewe kwa wenyewe.

MWISHO