Thursday, January 16

MAWAZIRI WAKIKABIDHIA MAKABIDHIANO YA MAJUKUMU YA KAZI PAMOJA NA ILA YA CHAMA CHA MAPINDUZI BAADA WIZIARA KUGEIWA

Baadhi ya Wafanyakazi walioshuhudia Makabidhiano ya Majukumu ya kazi ya Wizara pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi , kati ya Wizara ya Afya zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto, huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, akimkabidhi Majukumu ya kazi ya Wizara pamoja ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma, huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, akiagana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma,baada ya kumkabidhi Majukumu ya kazi ya Wizara pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi, huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma,akizungumza baada ya kukabidhiwa Majukumu ya kazi ya Wizara pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi,huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar ,(kushoto ) ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Anna Athanas Paul na (kulia) Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.

Na Khadija Khamis- Maelezo Zanzibar

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema maendeleo ya ustawi wa jamii yanahitaji jitihada na mashirikiano kwa watendaji wote ili kufikisha huduma za jamii kwa wakati.

Amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ina jukumu kubwa la kusimamia ustawi wa jamii pamoja na kushughulikia vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto.

Waziri Mazrui ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja wakati wa hafla ya kumkabidhi Majukumu ya kazi ya Wizara pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Mhe. Riziki Pembe Juma.

Amesema  mashirikiano ya pamoja na watendaji yatasaidia kuleta maendeleo kwa jamii ikiwemo kuwapa wananchi stahiki za pencheni  jamii kwa wakati pamoja na kushughulikia matatizo mbali mbali yanayowakabili wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukatili na udhalilishaji .

Nae Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Mhe. Riziki Pembe Juma amesema atatekeleza majukumu ya Wizara yake kwa kushirikiana na wafanyakazi wa wizara hiyo ili kuhakikisha  wanasimamia majukumu yao kwa lengo la kuleta ufanisi  .

Alifahamisha kuwa mashirikiano ya pamoja kwa wafanyakazi yatasaidia kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya kuleta maendeleo na ustawi bora kwa jamii.

Nae Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh amesema atashirikiana na wafanyakazi ili kuzitatua changamoto mbali mbali zilizopo katika wizara hiyo ili huduma zitolewe kwa ufanisi.

Alisema kufanya hivyo kutasaidia kuwapatia wananchi huduma  bora pamoja na kuzitatua changamoto ndogo ndogo zilizopo .

Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Watoto, Idara ya Jinsia na Watoto, Mohamed  Jabir amesema  Idara inashughulikia na kusimamia  haki za wanawake na watoto, watu wenye mazingira magumu pamoja makundi maalum.

Amesema Idara inawajibika kuwawezesha katika masuala ya elimu sambamba na  kuratibu mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Hivi karibuni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi alifanya mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi ambapo miongoni mwa Wizara iliyofanyiwa mabadiliko ni pamoja na Wizara ya Afya.