Thursday, January 16

HABARI PICHA: ZANTEL wakutana na mawakala ya huduma ya EzyPesa Kisiwani Pemba

MKUU wa Kitengo cha huduma za kifedha kutoka Zantel Moses Alphonse, akifungua mkutano wa mwaka wa mawakala ya huduma ya EzyPesa Kisiwnai Pemba, mkutano uliofanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba.
AFISA wa EzyPesa kutoka Zantel Eunice Alelyo, akiwasilisha mada juu ya faida za huduma ya EzyPesa na Lipa kwa Simu, katika mkutano wa mwaka wa mawakala wa huduma ya EzyPesa Kisiwani Pemba, mkutano uliofanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba
BAADHI ya mawakala wa huduma ya EzyPesa Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini mkutano wa mwaka wa mawakala hao, mkutano ulioandaliwa na kitengo cha EzyPesa kutoka Zantel na kufanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba
MENEJA wa Zantel Bernadetha Israel, akiwasilisha mada juu ya sheria za utakatishaji fedha na kuzuia Uhalifu, wakati wa mkutano wa mwaka wa mawakala wa huduma ya Ezypesa Pemba, mkutano uliofanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba
AFISA wa Mauzo na usambazaji kutoka Zantel Mwajuma Michael Mwanga, akiwasilisha mada ya Mimina na usambazaji kwa mawakala wa huduma ya EzyPesa Pemba, katika mkutano wa mwaka wa watoa huduma hiyo mkutano uliofanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba
MENEJA wa Huduma kwa wateja kutoka Zantel Fatma Khalfan, akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mawakala wa huduma ya EzyPesa Pemba, mkutano uliofanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba
AFISA wa EzyPesa kutoka Zantel Eunice Alelyo, akikabidhi zawadi kwa mawakala bora wa mwaka 2020/2021 wa huduma ya EzyPesa Pemba, mkutano uliofanyika ukumbi wa Samai Gombani Chake Chake Pemba

 

.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)