NA FATMA HAMAD PEMBA.
ZAID ya Shilingi milioni miamoja zimetengwa na taasisi ya SOS Zanzi bar kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao ni wajasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha na kutimiza ndoto zao kupitia biashara ndogo ndogo.
Meneja miradi wa Shirika la SOS Kisiwani Pemba Abdalla Omar, amesema taasisi hiyo imetenga kiasi hicho cha fedha ili kuwasadia vijana katika nyanja tofauti ikiwemo Uvuvi. Biashara na Kilimo hasa katika kuelekeza nguvu katika uchumi wa Bluu.
‘’Tunataka kuwawezesha vijana ili weweze kujiajiri wenyewe jambo ambalo litawaepusha kujiingiza katika vikundi viovu’’ alisema meneja Abdala.
Aidha alieleza kuwa fedha hizo zitawasaidia vijana kufanya miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo itawapatia kipato kitakachowasaidia katika familia zao.
Hivyo meneja huyo amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo za kimaendeleo ili waweze kuondokana na umaskini uliokithiri.
BaadhiyawadaukatikaKikaohichowalishauriserikalikufuatiliailimiradiyakuwawezeshavijanapamojanakuwapatiataalumasahihiyauendeshajinausimamiziwamiradi.