MKURUGENZI wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, kutoka Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Hanifa Ramadhan Said akizungumza katika mkutano wa wazi wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria huko katika shehia ya minazini Jimbo la Mtambile NAIBU Mrajis wa Ardhi Asha Suleiman Said, akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na wananchi wa shehia ya minazini Jimbo la Mtambele Wilaya ya Mkoani, katika mkutano wa wazi wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria. MWANASHERIA kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Safia Saleh Sultani akijibu hoja za kisheria za wananchi wa shehia ya Minazini Jimbo la Mtambile Wilaya ya Mkoani, katika mkutano wa wazi wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria. Asila Abdalla Ali mkaazi wa Minazini akiuliza swali katika mkunao wa wazi wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria, mkutano ulioandaliwa na Idara ya katiba na msaada wa kisheria Zanzibar, mkutano uliofanyika katika shehia ya Minazini Jimbo la Mtambile BAADHI ya wananchi wa shehia ya Minazini jimbo la Mtambile Wilaya ya Mkoani, wakifuatilia kwa makini Mkutano wa wazi wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria, ulioandaliwa na Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Zanzibar. AFISA Sheria kutoka Idara ya Msaada wa Kishefria Zanzibar Salma Suleiman Abdulla, akizungumza katika mkutano wa wazi wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria, mkutano uliandaliwa na idara ya katiba na msaada wa kisheria Zanzibar .(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA). Share