Thursday, January 9

Mawakala wa Eazypesa wakumbushwa wajibu wao wa kazi.


NA ABDI SULEIMAN.

WATOA huduma katika mitandao ya kutowa Fedha Kisiwani Pemba, wametakiwa kuhakikisha wanafuata sheria zote za utakatishaji wa fedha, ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza katika suala hilo.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Zantel, Bernadetha Israel wakati alipokua akiwasisha mada sheria za utakatishaji fedha na kuzuia uhalifu, kwa wamakala wa wanaotoa huduma za EzyPesa Kisiwani Pemba.

Alisema matatizo mengi yamekua yakijitokeza katika suala zima la utakatishaji wa fedha, ikiwa ni pamoja na kutumika kwa wizi na uhalifu.

“Siku hizi kuna sms zinatumwa, tuma pesa kwenye namba hii, hao ni wahalifu na unapotumiwa lazima uwe makini nao na wewe unaweza kuituma Zantel tu”alisema.

Alieleza kuwa ni vyema kwa mtaka huduma kuonyesha utambulisho wake, ikiwemo kitambulisho cha Mtanzania ikiwa ni mwenyeji wa nchi na sio kudai huduma za kifedha na muhudumu akakubali moja kwa moja tu jambo ambalo linaweza kumuingiza katika matatizo yasiokuwa na msingi.

Aidha alisema ulimwengu hivi sasa unaenda kwenye digitali, serikali malipo yake yote yanatakiwa kufanywa katika miamala ya kibenk au mitandao ya simu, lazima kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa sana.

Akizunguzmia kitengo mapato, meneja huyo alisema kuna mawakala wanafanya udanganyifu kwa kuwakata fedha wateja wao, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa kufuata sheria na ukweli.

Naye Afisa wa EzyPesa Eunice Alelyo, alisema lengo lao ni kuogeza minara, ili iweze kwenda vizuri, kwani mwaka huu wamekusudia kuboresha mambo mengi kwa lengo kutoa huduma bora kwa kuongeza huduma ya lipia malipo ya serikali.

Alisema uwepo wa huduma bora inachangia kwa kiasi kikubwa chachu ya maendeleo nchini, huku akielezea faida mbali mbali zinazopataikana kupitia lipa kwa simu.

“Huduma ya lipa kwa simu ni moja moja ya huduma nzri na rahisi sana, huduma inamfanya mfanyabiashara kutokutembea na pesa mkononi, imeweza kurahisisha mambo mengi kwa muda mfupi”;alisema.

Naye Mkuu wa huduma za kifedha Moses Alphonse, alisema lengo la mkutano huo ni kukumbushana kuhusu utaratibu na miongozo ya huduma za EzyPesa na huduma nyengine.

Katika hatua nyengine nae afisa mauzo na usambazaji kutoka Zantel Mwajuma Michael Mwanga, aliwataka watoa huduma hao kuhakikisha usajili zote za wateja zinapaswa kufanywa kwa kutumia alama za vidole pamoja na kuwa na vitambulisho halali vya mteja.

Kwa upande wao mawakala wa huduma za EzyPesa, aliitaka kampuni ya Zantel kuangalia jinsi ya utoaji wa huduma zitakazo kidhi mahitaji ya watumiaji wa mtandao huo.

Hata hivyo mawakala hao wameitaka kampuni hiyo, kuhakikisha inaendana na ushindani wa biashara uliopo hivi sasa katika vifurushi vyake vya dakika, MB na sms kama ilivyo mitandao mengine nchini.

MWISHO