Wajumbe katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima wanaoishi majumbani wakifuatilia kongamano la kuchangisha futari kwaajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taasisi ya kusaidia mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya kusaidia mayatima waishio majumbani Tanzania Taqwa Ophrans Trust dkt. Salha Mohammed Kassim akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar mama Zainab kuzungumza na kuchangisha futari Kwa ajili ya watoto mayatima waishio majumbani,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu akizungumza katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya watoto yatima waishio majumbani huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar,hafla hiyo imeandaliwa na Taasisi ya kusaidia watoto mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust.
Wajumbe katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima wanaoishi majumbani wakifuatilia kongamanola kuchangisha futari kwaajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taasisi ya kusaidia mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu (kulia) Akimkabidhi picha maalum mwenyekiti wa Taasisi ya kusaidia mayatima waishio majumbani Tanzania Taqwa Ophrans Trust ambayo aliinunua mweneyekiti huyo Kwa thamani ya shilingi laki 5 ya kitanzania ikiwa ni mchango wake katika kusaidia futari kwaajili ya mayatima waishio majumbani wakati wa kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taqwa Ophrans Trust huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mwandishi wa habari gazeti la Zanzibar Leo Juma Mmanga akiendesha zoezi la kuuza Kwa mnaada ikiwa ni Harambee kuchangisha futari kwa ajili ya watoto mayatima waishio majumbani wakati wa kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima hao lililofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu (katikati) akipokea picha maalum kutoka kwa mshereheshaji wa mnada Juma Mmanga mara baada ya kuinunua picha hiyo Kwa thamani ya shilingi milioni moja ya kitanzania ikiwa na mchango wake Kwa ajili ya futari ya watoto mayatima waishio majumbani wakati wa kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya watoto hao lililofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zainab Kombo amewataka waislamu pamoja na wapenda furaha na faraja kujitokeza kuiunga mkono Taasisi ya Taqwa Orphans Trust Tanzania , kwa kutoa ufadhili na kudhamini watoto yatima wanaowasimamia kwa lengo la kuwajengea uwezo madhubuti wa kuwahudumia vijana hao.
Akiyasema hayo katika Ukumbi wa Gorden Tulip wakati wa kongamano la kuchangisha Iftar kwa watoto yatima waishio Majumbani mwao.
Amesema jamii iendelee kushajihishana kutoa hasa katika kipindi cha Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani na si kwa Taasisi ya Taqwa pekee bali na Taasisi nyengine zinazoshughulikia Watoto yatima kufanya hivyo kutasaidia kuwapa faraja na ni njia moja wapo ya kufanya biashara na Mola Muumba hakika biashara hii haina hasara
Mama Zainab amesema atahakikisha anashirikiana na Taasisi hiyo, hatua kwa hatua katika kufanikisha shughuli za kila siku za kuwahudumia vijana hao.
Aidha amesema amefurahishwa kwa fikra ya kuanzisha taasisi hii ambao imesimamiwa na kutekelezwa na wanawake kwa hakika wanawake hao sio chemchem ya upendo na huruma bali ndio walezi wa jamii hii,na ni kimbilio la wenye dhiki na waliokosa furaha na pia ni mbegu bora ya amani katika nchi yetu.
Nae Mwenyekiti na Taqwa Orphans Trust Tanzania Dr Salha Mohamed Kassim alisema lengo la Jumuiya hii ni kuwapa furaha watoto yatima walio majumbani mwao kwa kuwapatia huduma za msingi za kijamii ikiwemo chakula, huduma za afya, elimu pamoja na shughuli za Iftar kwa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani.
Alifahamisha kwamba Taasisi ilifanya utafiti wa kujuwa jinsi ya kuwapa malezi bora yenye furaha watoto yatima wakagundua kwamba ni kuishi na familia zao zenye udugu wa damu ndio watapata faraja zaidi kuliko kuwatenga .
“ Malezi na Makuzi bora kwa watoto yatima ni kuishi na familia zao zenye udugu wa damu ambazo zinaleta upendo na faraja na ni silaha muhimu ya watoto pamoja na kufuata mila silka na tamaduni zao jambo ambalo linajenga imani kubwa kwa watoto hao na kuridhika , kuliko kuwatenga “alisema Dr Salha.
Akitoa wito kwa waumini kujitokeza kwa wingi kuwachangia watoto hao kwa ajili ya kuitafuta kheri ya hapa duniani na kesho ahera hata kwa kitu kidogo mtu ulichonacho kitasaidia .
Taasisi ya Taqwa Orphans Trust Tanzania imeanzishwa na wanawake wa kiislamu katika mwaka 2011 na Makao Makuu yake yapo Dar-es –salamu, hadi sasa wameweza kufikisha futari kwa familia 1593.