Saturday, January 4

WAFANYABIASHARA Pemba watakiwa kuitumia NMB ili waweze kunufaika na benki hiyo.

NA ABDI SULEIMAN.

WAFANYABIASHARA wametakiwa kupitisha Fedha zao katika bank ya NMB ili kuweza kunufaika na mikopo mbali mbali inayotolewa na bank hiyo.

Wito huo umetolewa na Meneja mwandamizi kutoka kitengo cha biashara NMB Tanzania Christopher Mgani, wakati akifungua mkutano wa wanafanyabiashara wanaotumia benki ya NMB Pemba, uliofanyika mjini chake chake.

Alisema endapo wanafanyabiashara hao watakapokopa katika bank hiyo na kujenga uwaminifu wa kurudisha fedha kwa wakati, wataweza kujijengea mazingira mazuri ya kuendelea na mikopo kila wanapohitaji.

“Awali wafanyabiashara walikuwa wakipata Milioni 50 sasa baada ya maboresho imepanda hadi kufikia 75 Milioni, hii ni kumsaidia kuongeza biashara yake kuwa kubwa,”alisema.

Aidha alisema bank bado inaendalea kujikita katika utoaji wa huduma mbali mbali ikiwemo kilimo, biashara, mikopo na wajasiriamali.

Naye kaimu meneja wa biashara za NMB Zanzibar Naima Said Shaame, alisema lengo la klabu za wafanyabiashara ni kuhakikisha bank ya NMB na wateja wanakua pamoja kila mwaka kupata kujua changamoto zao na kupewa mrejesho.

Aidha wanathamini wafanyabiashara hao kwani bila ya wao hakuna NMB, na kuahidi kuwa karibu sana na wateja wao siku zote ili kuona wananufaika na huduma zilizokuwa bora zaidi.

“Sisi kama bank tumekua karibu sana na wateja wetu ndio maana leo hii tumeamua kukutana nayi katika kujadiliana mambo mbali mbali ili kuona munaendelea kutumia bank yenu,”alisema.

Akitoa ufafanuzi wa maswali yanayoulizwa na wadau wao kuhusiana na mikopo, alisema lengo ni kuwainua wateja wao na sio kuwakandamiza au kuwaonea pale wanapochukua mikopo.

Kwa upande wake meneja wa NMB Tawi la Pemba Hamad Mussa Msafiri, alisema bank hiyo inazidi kuwa karibu na wafanyabiashara, wakulima na wafugaji kwa ajili ya kuwapatia huduma bora.

Akitoa maelezo mdau wa NMB kutoka mahakamani, hakimu wa mahakama ya Mkoa Chake Chake Luciano Makoye Nyengo, alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi inamalengo makubwa ya kutanua biashara na ndio maana masoko mengi yanajengwa kwa ajili ya wafanyabiashara.

Aidha aliwataka watendaji wa bank kutokupokea nyaraka isiyokuwa na stakabadhi ya malipo kutoka mahakamani kwa ajili ya masuala ya mikopo.

“Munapofika mahakamani munapaswa kulipa kulingana na bei stahiki iliyowekwa na mahakama kulingana na kiwango cha huduma zinazohitajika,”alisema.

kwa upande wao wafanyabiashara ambao wateja wa benk ya NMB, wameomba kupunguzia riba kwenye mikopo ili waweze kukopa kwa wingi ndani ya benk hiyo, pamoja na kupatiwa elimu ipasavyo juu ya fomu za mikataba ya mikopo.

Waliiyomba serikali kutanua huduma za malipo ya serikali kulipwa katika taasisi nyengine za kibenk ikiwemo banka ya NMB ili kupunguza msongamano ndani ya bank ya PBZ.