NA ABDI SULEIMAN.
BAADHI ya wananchi wa Shehia ya Minazini Jimbo la Mtambile na shehia ya kwendwa jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wamesema licha ya barabara ya Ole-Kengeja kutumia lakini bado hadi sasa baadhi yao hawajalipwa fidia ya nyumba zao zilizobomolewa ili kupisha ujenzi huo.
Wamesema sasa unafika mwaka wa tatu au wan ne bado kwenye account walizotakiwa kufungua, hakuna hata senti moja iliyoingia huku wengine wakihangaika kutafuta hifadhi kwa jamaa zao.
Wakitoa maoni yao katika mkutano wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya kisheria, ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, huko katika skuli ya msinbi Minazini.
Khamis Mohamed mkaazi wa Jundamiti, alisema barabara ya ole kengeja hadi leo kuna wananchi bado hawajalipwa fedha zao, licha ya nyumba zao kubomolewa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara hiyo.
“Yupo mzee Ali Salim Ali tokea kuvunjwa nyumba yake hadi sasa emkua akihangaika na sehemu ya kukaa, huku baadhi ya maeneo Unguja wananchi wameshalipwa”alisema.
Akizungumzia suala la vyeti vya kuzaliwa, alisema imekua ni tataizo wazee wenye umri mkubwa kupata vyeti hiyo kutokana na mashari yaliyopo hivi sasa.
Naye Mohamed Juma Khamis mkaazi wa Nanguji, alisema bado wanakilio kikubwa juu ya malipo ya vipando vyao katika barabara ya Ole-Kengeja, licha ya kufungua Account benk hakuna kitu kilichoingizwa.
Hata hivyo aliyombo serikali ya awamu ya nane kuwangalia kwa jicho la huruma kwani wamekua wakisumbuka kutafuta sehemu za kukaa, huku mvua zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.
Kwa upande wake Rajab Salim Omar, ameitaka idara ya katiba na msaada wa kisheria, kuhakikisha inandaa siku maalumu kwa ajiliya kutoa elimu ya sheria kwa wananchi wa kiwania na minazini.
Alisema elimu hiyo itaweza kufunua vichwa vya wananchi hao, kwani kumekua na mambo mbali mbali yanafanyika na kutokujuwa hatma yake, wala sehemu ya kwenda kudai haki zao.
Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema kesi nyingi za udhalilishaji zinafeli au kufa kwa sababu jamii inashindwa kwenda kutoa ushahidi mahakamani wanapotakiwa.
“Haya matukio makosa mengi huanzia kwa jamii, pale mtoto anapobakwa kwa kutokutaka kutoa ushahidi, jambo ni kosa kisheria na linapelekea kumnyima haki zake”alisema.
Naye naibu Mrajis wa Ardhi Asha Suleiman Said, alisema migogoro ya ardhi imekua mingi katika jamii, kutokana na ukosefu wa elimu na uwelewa wa kisheria baadhi ya wananchi wanakosa kabisa haki zao.
Kwa upande wake mwanasheria kutoka kituo cha huduma za sehria Zanzibar Tawi la Pemba Safia Salehe Sultani, alisema kesi za ubakaji hazina zamana, huku akiwataka wananchi kuachana na muhali pale wanapoitwa mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Naye msaidizi wa sheria jimbo la Kisiwani Salehe Mussa Alawi, aliwataka wananchi kuwatumia wasaidizi wa sheria pale wanapokua na matatizo yao.