NA ABDI SULEIMAN, BABATI.
SUALA la Uhifadhi wa Wanyamapori kwa wananchi wa kijiji cha Sangaiwe Wilaya ya Babati Mkoa wa Mnyara, imeweza kuondosha shida ya kuchangishana shilingi elfu 20000, kwa kaya kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kusomea watoto wao.
Wamesema kwa sasa suala la kupigana michango ya fedha, limeondoka kila ujenzi unapotaka kuanza, kwani fedha hizo hutolewa na jumuiya ya Hifadhi ya jamii Burunge WMA.
Wakizungumza katika ziara ya chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), walipotembelea na kuangalia shuhuli za uhifadhi, utalii na kijamii pamoja na mapitio ya wanyamapori ya kwakuchinja, chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili wa shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID).
Mmoja ya wanakijiji hicho Venust Peter, alisema kabla ya WMA wanapotaka kufanya kitu kijiji hapo, lazima kuchangishana fedha na kiwango hakipatikani kwani wengine hukimbia kaya zao.
Alisema kwa sasa shuhuli zote za ujenzi hutolewa tenda na watu hupata pesa na mradi kukamilishwa kwa wakati na wananchi hawasumbuliwi tena kuchangia.
“Uhifadhi umetupatia kipato katika kijiji chetu, baada ya elimu tunalima na tunaendelea kuhifadhi wanyamapori, tulikua vijiji vitano sasa vimekua vijiji 10”alisema.
Naye Stellm Thomas (57)alisema kabla ya uhifadhi ilikuwa ni shida sana kijijini kwao, kila ujenzi unakaribia lazima kila kaya kuchangishwa shilingi Elfu 20,000/=, sasa imekua ni tafauti na huku vijiji vya jirani vikitamani kunufaika nao.
Alisema kwa sasa hata watoto wanapata chakula skuli na matunda, kutoka katika hifadhi hiyo ya burunge, hali inayowafanya kusoma kwa umakini mkubwa sana.
Akizungumzia uwepo wa kituo cha kisasa cha zahanati, alisema akinamama wajawazito wanajifungulia kijijini kwao na wahatembei tena umbali wa kilomita 8 kufuata kituo cha afya.
“Mimi natamani sasa nirudi katika ujana wangu, tulikua tunaenda zaidi ya kilomita 8 kufuata huduma za afya, sasa shule ipo kijijini, zahanati ipo kijijini kila kitu kipo sawa”alisema.
Kwa upande wake Anastazia John Mwanso, alisema uhuifadhi umewasidia kuanzisha vikoba kwa akinamama, ambapo wanakopeshana na baadhi yao wanafanya biashara ndogo ndogo.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Singaiwe Nikodemas Mofulu, amesema wananchi wanajivunia uhifadhi walionao baada ya elimu waliopatiwa, kwani wanapata fedha nyingi kufuatia kutunza eneo la hifadhi ya jamii.
Alisema wanahoteli mbili hoteli na wanapata milioni 48 kwa mwaka, sambamba na kupunguza shida ya masafa marefu ya watoto kufuata huduma hiyo.
Mwenyekiti hifadhi ya jamii Burunge WMA Khamis Juma Mgimba, alisema Sangaiwe ni moja ya vijiji ambavyo vinamuingiliano mkubwa na kimepakana na hifadhi ya Tarangire, kina wanyama wengi tafauti vijiji vyengine vilivyopakana na hifadhi ya burunge.
MWISHO