Thursday, January 9

Fahamu dawa ambazo zinaweza kuwa hatari kwako

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, dawa hizo zinapoteza ufanisi wake kwa kasi ya kushangaza
Maelezo ya picha,Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, dawa hizo zinapoteza ufanisi wake kwa kasi ya kushangaza

Kula vyakula vya kukaanga ama vilivyo na mafuta mengi kunaweza kusababisha kuumwa na tumbo au kuvimbiwa.

Baadhi ya wanapokabiliwa na tatizo kama hilo hukimbilia duka la dawa na kupata vidonge vya kujitibu bila ushauri wa daktari.

Kununua dawa bila maelekezo ya daktari sio jambo geni muongoni mwa rais wa nchi za Afrika Mashariki.

Ijapokuwa nchi hizo zina utaratibu wa kudhibiti ununuzi bila ushauri wa daktari, maduka mengi ya kuuza dawa hayafuati utaratibu huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, dawa hizo zinapoteza ufanisi wake kwa kasi ya kushangaza kutokana na matumizi mabaya na yasiyo ya kukusudia ya antibiotiki.

Lakini dawa hizi zinaweza kuwa na madhara gani kwa afya zikitumiwa bila ushauri wa daktari?

Paracetamol

Watu wengi hutumia paracetamol kwa maumivu au homa.

Madaktari mara nyingi huagiza paracetamol kwa homa au maumivu ya mwili. Makampuni tofauti huuza kwa majina tofauti.

“Tunabainisha jinsi na kwa muda gani wa kula. Lakini baadaye wagonjwa hununua na kula tu wakati wana homa au maumivu ya mwili. Matokeo yake, inapoteza ufanisi wake wakati fulani” anasema mtaalamu mmoja.

Matumizi ya muda mrefu ya paracetamol au acetaminophen yanaweza kusababisha uharibifu wa ini.

Dawa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Matumizi yasiyodhibitiwa ya dawa za kuzuia maumivu au kushindwa kumaliza dozi kunaweza kusababisha hatari kubwa kwa mwili

Aspirin

Aspirin ni dawa muhimu sana lakini inaweza kuwa hatari ikitumiwa kiholela kwa sababu sio salama kwa kila mtu

Dawa hii inajulika kwa ubora wake wa hali ya juu ya kutuliza maumivu na wakati mwingine hutumiwa kutuliza homa.

Wazee, ambao wana magonjwa ya moyo- madaktari huwapa dawa hii kwa kipimo fulani. Ikiwa kuna madhara pia hufuatiliwa.

Madhara

Inaweza kusababisha chakula kisisagike vizuri hali ambayo inaweza kumsababishia mtu kupatwa na vidonda vya tumbo.

Usimpatie mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 16 asprin bila ushauri wa daktari.

Inaweza kuwafanya watoto kupatikana na ugonjwa hatari unaojulikana kama Reye syndrome ambayo inaweza kuathiri (ini au ubongo).

Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu na uvimbe huchangia ongezeko la hatari ya kupata maradhi ya moyo, utafiti umebaini.

Diclofenac na dawa zingin

dawa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Madaktari wanasema kuwa kununua dawa bila agizo la daktari imekuwa jambo la kawaida

Watu wengi hutumia dawa mbalimbali za kutuliza maumivu ya mwili, maumivu ya mguu au maumivu ya kichwa. Hasa ikiwa unapata maumivu kwa sababu yoyote, kununua ibuprofen au diclofenac kutoka kwa maduka ya dawa na kuanza kuitumia.

”Inaweza kusababisha matatizo ya tumbo, kuharibu tumbo, na kusababisha kutokwa na damu. Mikono na miguu ya watu wengi hutoka maji, huvimba,” anasema Dk Maula.

Matumizi ya muda mrefu ya madawa haya yanaweza kusababisha kutokwa na damu ya utumbo. Baaadhi ya watu wanakabiliwa na mmeng’enyo mbaya wa chakula, wana vidonda, na wanaweza kuwa waraibu wa dawa za kulevya.

Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na kuvimbiwa.

Metronidazole

Dawa nyingine ambayo inatumiwa vibaya inafahamika kama metronidazole. Baadhi ya watu huzinunua bila maelekezo ya dakatari wakiwa na maumivu ya makali ya tumbo kwani pia ni aina ya dawa ya kutuliza maumivu.

Madhara ni pamoja na upele na kuvimbiwa. Kisha yanafuatiwa na shida nyingine kama kutokwa na damu katka sehemu za siri Mgonjwa anapata choo kigumu,ambacho kinasababisha maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.

Dawa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Shirika la Afya Ulimwenguni linasema unyanyasaji wa viua vijasumu unaweza kuua watu milioni 300 ulimwenguni ifikapo 2050

Dawa zingine hatari zaidi

Baadhi ya watu hununua dawa za tezi au steroid kutoka kwa maduka ya dawa kwa matatizo ya koo. Lakini matatizo ya dawa hizo kiholela yanaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya.

Madaktari wa kitaalam wametoa ushauri juu ya matamizi ya dawa hizi.

  • Ikiwa una tatizo la dharura sana kama vile maumivu, hata ukinunua dawa moja au mbili za dharura kutoka kwa duka, unahitaji kushauriana na daktari haraka iwezekanavyo.
  • Hakuna antibiotics inapaswa kumezwa kwa ushauri wa wafanyakazi wa maduka ya dawa.
  • Ukiwa na homa, maumivu ya tumbo au tatizo lolote la kimwili, ushauri wa daktari unapaswa kuzingatiwa kabla ya kumeza dawa yoyote kiholela.
  • Angalia madhara na muda wa dawa yoyote kabla ya kutumia.
  • Wakati wa kununua dawa, nunua dawa kwa kuzingatia maagizo ya daktari.