NA ABDI SULEIMAN.
WAZIRI wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis, amesema serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa mbole kwa wakulima, chakushangza mbole hizo haziwafiki walengwa badala yake zinasafirishwa hadi Tanga na kuuzwa Dar es Salaam.
Alisema hilo halitaki tochi kwani wakulima wengi bado wanaendeleo kulia juu ya suala zima la mbolea, wakati serikali imetoa mblea bure kwa ajili ya kuwapatia wakulima ili kuwapunguzia mzigo, jambo ambalo liko tafauti na malengo ya serikali.
Waziri huyo aliyaeleza hayo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua shuhuli za kilimo zinazofanywa na vijana kupitia mradi wa Viungo, mboga mboga na matunda (Viungo Project) unaotekelezwa na taasisi tatu PDF, CFP na TAMWA kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.
Alisema vijana wameshakuwa wastahamilivu wakubwa na kujikita katika kilimo, ikizingatiwa kilimo hupotezi bali unaekeza kwani utajiri shambani na sio kijiweni.
Aliwataka vijana kutokurudi nyuma licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali, Serikali yao bado iko pamoja nao kwa kuhakikisha inatatua baadhi ya changamoto zinazowakabilia kwa kushirikiana na taasisi binafsi.
Aidha waziri huyo alisema miradi mingi imeletwa na watu wamevuruga fedha zake, ikiwemo MACCEP, PADEP na hakuna kilililotekelezwa, huku akitabanahisha miradi itakayokuja mipya hakutakua na taasisi mpya zaidi ya kuwaendeleza vijana waliojiajiri wenyewe katika shuhuli mbali mbali.
“Miradi mingi imekuja watu wameharibu fedha, kila mradi unaona vikundi vipya vinaundwa baada ya kuviendeleza vilivyopo, vikundi hivyo wengi wao ni watoto wao hapo hakua na mradi”alisema.
Hata hivyo alimtaka mdhamini wa Wizara hiyo, kuhakikisha vijana wa kilimo katika bonde la Nyange wananufaika na miradi hiyo na sio kuanzisha vikundi vipya.
Alisema serikali inapoteza fedha nyingi mwisho hakuna kitu kilichofanywa, hakuna nchi yoyote duniani inayofanya kazi kwa kuwa watu kijio, Serikali imeamua kwa sasa yoyote anayeamua kufanya kazi nao, lazima kumjuwa nani na wapi anapofanya kazi.
Hata hivyo alisema amefurahishwa na vijana hao, kujitoa kwao na kujikubalisha kuingia katika kilimo, kama ni vijiwe wameshakaa sana na haviwasaidii.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Mradi wa Viungo kutoka CFP Sada Segeja, alisema kikundi cha mjini Ole Bonde la nyange walikua ni 25na kubakia 15, ambapo wakulima wamelima eneo zaidi ya ekari 15 katika kilimo cha tungule.
Alisema waliweza kutoa bolea polo 300 kila polo lina kilo 50, lengo ni kuwapunguzia ugumu wakulima hapo katika shuhuli zao za kilimo.
Naye mkulima wa Tungule Juma Omar, alisema kwa sasa wafanyabiashara wanawafuata shambani na hakuna tungule inayochumwa kama wahajakubaliana bei mwanzo.
Ahata hivyo alisema bado wanakabiliwa na changamoto kubwa, katika suala la maji ikizingatiwa kipindi hiki ni jua kali pamoja na kukosa wataalamu wa kilimo hali iliyofanya baadhi ya mitungule kunyauka.
MWISHO