Thursday, January 9

SAUTI: FAMILIA YA ABDALLA HUSEIN RASHID YATOA YA MOYONI

Familia ya kijana Abdala Husein Rashid mwanafunzi wa darasa la kumi skuli ya kinyasini Wete Pemba mwenye ulemavu wa viungo yaomba msaada kwa wasamaria wema kupatiwa kigari kwa ajili ya
kuendea skuli.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama mzazi wa kijana huyo Time Kombo huko nyumbani kwake kwale gongo iliopo wilaya ya wete mkoa wa Kaskazini Pemba amesema kigari alicho nacho ni chaji hivyo maranyingi humzimikia njiani hakimfikishi skuli na hukwama njiani kwenye milima.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa skuli ya kinyasini Asha Mbarouk Rashid nayeye hakuacha kuelezea changamoto za kijana huyo .

Abdala Husein Rashid anasoma darasa la kumi Skuli ya sekondari kinyasini na anaishi kwale gongo ambapo ni kilomita 2.5 kutoka nyumbani kwao hadi Skuli anakosoma.