NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali ameziomba taasisi pamoja na watu wenye uwezo kutoa mashirikiano katika kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili waweze kutekeleza Ibada hio katika hali ya furaha na amani.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito huo wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa chakula kwa watu wenye ulemavu wa ngozi uliotolewa na Jumuiya ya kimataifa ya maendeleo Zanzibar ZIDO huko Skuli ya madungu Chake Chake.
Amesema ZIDO imekuwa mfano bora katika kutoa misaada kama hio katika makundi mbali mbali hivyo ni vyema na wengine kuiga mfano huo.
Kwa upande wao Rais wa Jumuiya hio bibi Rehana Meral kutoka CANADA na Mkuu wa Taasisi hio kwa upande wa Zanzibar Makame Ramadhan wamesema ZIDO itahakikisha inashirikiana na Serikali bega kwa bega katika kusaidia wananchi ili waweze kuishi maisha bora.
Nao wanajumuiya ya watu wenye ulemavu wa ngozi wameipongeza taasisi hio kwa msaada wao lakini pia wameiomba ZIDO pamoja na wahisani wengine kuangalia uwezekano wa kuwasaidia katika musuala ya afya ili waweze kujikinga na maradhi mbali mbali yanayoweza kuwapata.
Msaada huo wa chakula ni pamoja na mchele, maharage, unga wa ngano, sukari ,tende na Mafuta ya kupikia.
KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI YA VIDEO.