Saturday, January 4

Mabadiliko ya tabia nchi yaathiri ziwa burunge.

NA ABDI SULEIMAN.

KATIBU wa WMA hifadhi ya Jamii Burunge Benson Mwaise, amesema kutokana na madadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kuikumba dunia hivi sasa, wana haja ya kufanya jitihada za msingi ili kuona ziwa burunge halifiki kukauka ispokua ni maumbile.

Alisema wanajitahidi kushirikiana na wadau mbali mbali, ili kuona ziwa hilo halikauki na wakulima, mifugo na shuhuli za uvuvi zinaendelea kufanyika na wananchi wanaozunguka ziwa hilo wanaendelea kunufaika nalo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), walipotembelea na kuangalia shuhuli za uhifadhi, utalii na kijamii pamoja na mapitio ya wanyamapori ya kwakuchinja, chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili wa shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID).

Alivitaja baadhi ya vijiji zinavyonufaika ni sangaiwe, mwada, ngolei na vilima vitatu, ambapo ziwa hilo linapokauka wanyama kutoka Hifadhi ya Tarangire kuja burunge inakuwa kubwa na kwenda katika mashamba ya watu na kuathiri sana.

Aidha alisema licha ya mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo hivi sasa, tatizo jengine linalopelekea ziwa burunge kukauka ni mito inayoingiza maji ziwani humo kupasuka na maji ya Ziwa burunge kwenda ziwa Manyara.

“Zile Mvua kubwa zilizowahi kunyesha zilileta madhara, sehemu ya mtu unaingiza maji chanali yake ikamomonyoka njia zake za upande mmoja na maji kuwenda upande wa ziwa manyara, maji mengi yanatokea tarangire na kuingia humo”alisema.

Katibu Mwaise alisema wananchi wananufaika na WMA wanategemea kupata maji na watalii, hufurahia monekano wake zaidi pale alfajiri jua linapochomoza, huku wakiendelea kulitunza ipasavyoa kwa munafaa ya sasa na baadae.

“Ilifika wakati wadau wetu tukataka kutusaidia skaveta kwa ajili sehemu inayopitisha maji, kwani zina linapokauka idadi ya wanyamapori kutoka hifadhi ya Tarangire inakuwa kubwa na changamoto za HWC sio rahisi kudhidhibiti”alisema.

Aliongeza kuwa ziwa linapokua na maji vijiji vichache vinabakia ikiwemo Sangaiwe, kokoi na Vilima vitatu, linapokauka kokoi, ngolei, minjingu na vilima vitat vinakubwa na HWC.

Akizungumzia suala la mafanikio, alisema ziwa hilo linatoa fursa kubwa kwani wanampango wao matumizi unaonyesha kiasi gani cha wavuvu wanafanya shuluzi za uvuvi, aina ya zana wanazotumia mitumbwi na nyavu ni zile zinazotambuliwa na serikali.

Kwa upande wa ulinzi, alisema upo kwani hutumia vikosi vyao ili kuhakikisha wavuvi naatumia zana nzuri na kuhakikisha amzingira yanatunzwa.

Nao wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi ya jamii Burunge, wamewashukuru viongozi wa hifadhi hiyo kwa juhudi mbali mbali wanazozichukua ili kuona ziwa hilo linaendelea kuwasaidia wananchi.