NA ABDI SULEIMAN.
WAZIRI wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis, amesema dhamira ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara hiyo, ni kuwatambua wale wote wanaofanya shuhuli mbali mbali zinazohusu taasisi zao.
Alisema lazima kuzitambua taasisi zinazofanya shuhuli zinazofanana, ili kusudi kujua nguvu kazi yao nyengine iki sehemu gani na kiwango gani.
Waziri Shamata aliyaeleza hayo wakati alipokua akizungumza na wanakikundi cha ukulima wa mbogamboga mbali mbali, kilichopo kijiji cha Vikunguni kinachojulikana mawazo yenu.
Alisema vipo baadhi ya vikundi vinapatiwa fedha kutoka kwa mashirika mbali mbali, ambayo yanachukuliwa dhamana na serikali lakini mwisho wasiku hakuna kitu kinachofanyika..
“Mambo ya hadithi hadithi sasa basi,lazima tujuwe umemsaidia nini na nani, uliyemsaidia shuhuli zake na wapi anapofanya, zipo vikundi vimepatiwa fedha na hakuna wanachokifanya”
Aidha Waziri huyo alisema, serikali serikali inaagiza mbegu za mpunga watu wanagawana na kuvuna hata hawajapanga, mwisho wa siku inalaumiwa serikali kwa kutokufikisha ppembejeo wakati wanazopewa wanazitumia vibata na hakuna kinachoonekana.
Hata hivyo aliwapongeza wakulima hao na CFP kwa kutafuta soko la papai, sambamba na kuwahamasisha wananchi juu ya matumizi ya mapapai.
Naye Meneja wa Mradi wa Viungo kanda ya Pemba Shaarif Maali, alisema mradi unatekelezwa na taasisi nne, kwa shehia 60 Unguja na Pemba, ambapo unashuhulikia wakulima 57970 na wamegawika makundi.
Alisema lengo ni kuongeza uzalishaji kwa wakulima na kutoa elimu, kwa kulima kutumia vikundi mbali mbali ili wananchi waweze kupata mapato.
Kwa upande wao wakulima wa kikundi cha Mawazo yenu, alisema changamoto kubwa inayowakabiliwa ni ukosefu wa maji kwa ajili ya kumwagilia mazao yao.
Walisema kwa sasa maji imekua ni changamoto kubwa kwao, baada ya kukauka kwa mabwawa ambayo hutumia au kuwasaidia katika umwagiliaji, huku maji ya zawa yakiwa mbali na wao.