NA ABDI SULEIMAN.
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya CHEMCHEM Walter Pallangyo, amesema wajibu wa sekta binafsi katika kusaidia uhifadhi wa bayoanuai na kulinda mapitio ya wanyamaporo (shoroba), ni kuhakikisha jamii inayozunguka eneo lililohifadhiwa wanakua na uwezo wa kutengeneza vyanzo vyao vya mapato, ambavyo vitawasaidia kufanya ujangili wa wanyamapori na uharibifu wa mazingira.
Alisema katika kutilia mkazo hilo Chechem, imelazimika kutengeneza vikundi vya akinamama vya kuweka na kukopa (vicoba), wanawake hukutana na kuzungumzia masuala ya uhifadhi na kuweka hakiba zao na kupata mikopo.
Alifahamisha kuwa wameweza kusaidia ukarabati wa madarasa na kujenga mapya, kwa skuli ambazo zimetawanyika katika shoriba ili kuwasaidia watoto, kupata elimu na kuacha kutapakaa mitaani na kuishia kufanya kazi zitakazopoteza thamani ya eneo la kwakuchinja.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya CHEMCHEM aliyaeleza hayo, wakati alipokua akiwasilisha mada juu ya wajibu wa sekta binafsi, katika kusaidia uhifadhi na ulinzi wa bayoanuai na korodoo za wanyamapori, kwa waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) kupitia mradi wa tuhifadhi maliasili kwa ufadhili wa shirika la USAID.
Kwa upande wa elimu, alisema wameweza kununua basi wanafunzi ili kwenda skuli na kurudi, kwa lengo la kuwavusha kutoka vilima vitatu kwenda kijiji cha minjingu, pamoja na kuwapunguzia adha wanawake kuingia katika jamanga ya kupata mimba na kutembea kilomita kufuata skuli15.
“Mwanzo wanafunzi lazima waamke alfajiri sana, njia wanayopita ndio muda wa wanyama kama fisi, samba na tembo kwenda ziwa manyara au tarangire, jambo ambalo lilikuwa likihatarisha maisha yao”alisema.
Hata hivyo alisema wametoa visaidizi 260 kwa watu wenye ulemavu, sambamba na kutoa elimu umuhimu wa kuhifadhi wanyamapori kwa watoto kwenye kijiji cha vilima vitatu na Sangaiwe.
Akiwasilisha mada juu ya wajibu wa sekta binafsi katika kusaidia uhifadhi nchini Tanzania, mchambuzi wa Sera kutoka TPSF Victoria Michael, ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wao na kuwashirikisha katika mambo mbali mbali, ikiwemo mchakato wabajeti kwa kukusanya maoni kutoka kwa wanachama wao.
Aidha alisema wamelazimika kujenga uwelewa, kwa sababu masuala ya uhifadhi wa wanyamapori, ni changamoto ambayo Serikali na wadau wa maendeleo pekee yake hawawezi kuifanya bila ya kushirikisha sekta binafsi.
“Shuhuli zote za uwindaji haramu, uhiribifu wa mazingira unafanywa na sekta binafsi, hivyo kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kuchukua tahadharia,”alisema.
Naye Dr.Elikana Kalumanga sekta binafsi ni muhimu sana katika suala zima la uhifadhi na bayoanuai, huku akihikisha kila taasisi inafuata sera na sheria zinazotaka.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) John Chikomo, alisema lengo la warsha hiyo ni kuongeza uwelewa kwa waandishi wa habari kujua majukumu ya taasisi zinazojihusisha na masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na bayoanuai.