Thursday, January 9

VIDEO:Makala maalum: Ujio wa ZIDO kisiwani Pemba na ugawaji wa futari.

 

NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.

Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa ukarimu na kutoa sana sadaka. Hii Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas  akisema: “Alikuwa MtumeMuhammad  (saw) ni mkarimu sana kushinda watu wote katika kufanya mambo ya kheri, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani. Kwani kuna fadhila kubwa unapotoa sadaka katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.

Katika kupata ujira huo  watu wengi ambao wamebarikiwa kuwa na uwezo ijapo mdogo hupendelea kufuata mwendo wa Bwana Mtume Muhammad , SAW  ili nao waweze kupata ujira huo .

Jumuiya ya Kimataifa ya Maendeleo Zanzibar ZIDO ambayo ipo huko Makunduchi Zanzibar  yenye makao makuu yake nchini Canada  ni Jumuiya ambayo imekuwa ikitoa misaada mbali mbali kama vile uchimbaji wa Visima, kusaidia upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye mazingira magumu, dawa Hospitalini pamoja na mahitaji mengine kadhaa,  ni kwa miaka kadhaa sasa ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhan huwa inajikita katika kutoa misaada ya chakula kwa ajili ya futari kwa watu mbali mbali ambao wanaishi katika mazingira magumu  katika Visiwa vya Unguja na Pemba,  ili kuhakikisha watu hao nao wanatekeleza ibada zao katika hali ya utulivu na amani. Huku wakitaraji kupata ujira mwema kutoka kwa Mola wao.

 

KUANGALIA MAKALA HAYA BOFYA HAPO CHINI.