NA ABDI SULEIMA.
MAAFISA wa mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Pemba, wamefanikiwa kukamata kete 1643 za unga unaosakiwa kuwa ni madawa ya kulevya, zikiwa juu ya dari huko Jondeni Mkoani Pemba.
Tukio hilo lilitokea Aprili 22, majira ya saa kumi na nusu jioni, huko Jondeni Wilaya ya Mkoani juu ya dari ya Nyumba ya mtuhumiwa Ramadhani Suleiman Juma.
Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, kamishna wa Uchunguzi Intelijensia na Operesheni, kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za Kulevya Zanzibar Khamis Bakari Amani, alisema kete hizo wamezikamata juu ya dari baada ya kufanya upekuzi ndani ya nyumba hiyo.
“Wakati waupekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa Ramadhani Suleiman Juma, keti 1643 zimekutikana zimeziweka juu ya dari,”alisema.
Aidha kamishna huyo alisema kwa sasa muhusika wa tukio hilo, yuko chini ya ulinzi na pale upelelezi utakapokamilika watahakikisha wanamfikisha katika vyombo vya sheria ili kuchukua hatua zaidi.
Hata hivyo aliwashauri Vijana, kuachana na dawa za kulevya, kutokana na sheria yeke imekua nzito na ngumu hivi sasa, kwani mtu yoyote atakaepatikana na dawa za kulevya kiwango kikubwa hukumu yake ni kifungo cha maisha.
Alisema tamaa ya siku moja isikusababishie ukafungwa kifungo cha maisha yako yote, hivyo wanapaswa kuaachana na kutafita kazi mbadala za kufanya, sambamba na kuitaka jamii kushirikiana na mamlaka ili kuwafichu wauza dawa za kulevya.
Wakati huo huo watendaji wa Mamlaka hiyo Pemba, wamefanikiwa kukamata mafurushi manne(4) na stiki 100 za Bangi huko Mahudusi Kengeja Wilaya ya Mkoani.
Mratib wa mamkala hiyo Pemba Omar Juma Mbarouk, alisema tukio hilo lilitokea Aprili 23 saa mbili na nusu Usiku, huku akiwataja watuhumiwa hao ni Kheri Makame Kombo (21) na Fumu Ali Makame (20) wote ni wakaazi wa Mwambe bwegeza.
MWISHO