NA ABDI SULEIMAN.
WANAUSHIRIKA wa Tushikamaneni kilichopo Kiuyu Wilaya ya Wete, wameshauriwa kufanya biashara zao kiutalii zaidi, ili kuweza kuwavutia wageni wengi zaidi wanapenda kuangalia bidha za mikono zinazofanya na wajasiriamali.
Alisema wizara hiyo inakusudia kulifanya eneo la Kiuyu kuwa eneo la biashara za kiutalii zinazofanywa na wajarimali wa eneo hilo, ili wageni waweze kunua na kuangalia bidhaa hizo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Zuhura Mgeni Othman, wakati alipokua akizungumza na wanakikundi cha Tushikamaneni kilichopo Kiuyu Wilaya ya Wete.
Alisema sasa wakati umefika kwa wajasiriamali wa Pemba kuachana na utengenezaji wa vitu vya asili kimazowea, badala yake kufanya kibiashara zaidi kwani soko la vitu hivyo kiutalii lipo.
“Sekta ya utalii ni kuba na pan asana imegusa mambo mengi, ikiwemo wafanyakazi za mikono za asili, vizuri sasa tukaimarisha biashara zetu kuwa za kitalii sasa”alisema,
Hata hivyo alisema lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha wajasiriamali wanaofanya shuhuli za ujasiriamali, kujikitaka katika suala la utalii katika biashara zao.
Akizungumzia suala la Sensa, aliwataka wanawake kujitayarisha kuhesabiwa wakati wa sense itakapo, sambamba kuwahamasisha waume zao kubakia majumbani siku hiyo itakapofika.
Kwa upande wake Afisa Utalii Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Ali Juma, alisema wageni wengi wanatembelea Zanzibar huvutiwa na shuhuli wanazozifanya wananchi ikiwemo kazi za sanaa.
Alisema watalii huvutiwa na kazi za sanaa ambazo zinafanywa na wananchi, kwani wanaweza kujivunia pesa kupitia sekta hiyo ya utalii.
“Hayo ipo haja kujiongeza katika mambo wanayoendelea kuyafanya, hivi sasa sio suala la kukata tamaa kwani soko la vitu vya ufinyazi kwa utalii lipo la kutosha”alisema.
Aidha alisema kamisheni ya Utalii Pemba, inajipanga kuhakikisha inalifanya eneo la Kiuyu kuwa ni eneo la kiutalii, kwa wananchi hao kuweka bidhaa zao eneo la chamanangwe na watalii kupita na kununua bidhaa hizo.
Katibu wa kikundi cha Tushikamane kilichopo kiuyu, Zalha Salum Hamad alisema kikundi chao kinakabiliwa na Changamoto mbali mbali mbali, ikiwemo ukosefu wa Charahani pamoja na soko la kuuzia bidhaa zao.
Alisema changamoto nyengine ni ukosefu wa sanduku la kuwekea fedha zao, kwani hivi sasa fedha zao hazipo katika mikono salama kutokana na ukosefu wa kasha hilo.
MWISHO