Thursday, January 16

WASAIDIZI wa Sheria Pemba watakiw akuwa wabunifu

 

NA ABDI SULEIMAN.

WASAIDIZI wa Kisheri Kisiwani Pemba, wametakiwa kuendelea kusaidia jamii na kuwa wabunifu, kubadilika kulingana na mazingira, katika utoaji wa huduma za msada wa kisheria kulina na matakwa ya jamii.

Wito huo umetolewa na Afisa Mdhamini Ofisi ya Rias katiba sheria utumishi wa umma na utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali, wakati akifungua mkutano warobo mwaka wa kuratibu masuala ya msaada wa kisheria uliofanyika Gombani Chake Chake Pemba.

Alisema iwapo wasaidizi wa kisheria wataendelea kutoa msaada wa kisheria kwa jamii, jamii itakuwa imepata mambo mengi ambayo walikuwa wakiyakosa.

Aidha alisema kila mmoja anawajibu na jukumu la kuwasaidia na kuwapatia elimu ya msaada wa kisheria jamii, ikiwemo wanawake, watoto, mirathi, ardhi ili kuona elimu inawafikiwa wengi zaidi.

“Lazima tuthamini juhudi zinazoendelea kufanywa na wasaidizi wa sheria, kupitia idara ya katiba na masaada wa kisheria Zanzibar, kwani wanafanya kazi kubwa katika kutoa elimu na kuwafikia wananchi wengi wanaohitaji elimu ya msaada wa kisheria”alisema.

Mdhamini huyo alisema vikao hivyo washiriki hujifungia na kutoa na mikakati itakayoleta mageuzi katika serikali jamii na wasaidizi wa sheria husika.

Alisema serikali inathamini juhudi na umuhimu wa watu wa msaada wa kisherai, sambamba na kuwapongeza kutokana na mambo mengi yanaonekana na yamebadilika kutokana na juhudi za wasaidizi hao.

Hata hivyo mdhamini huyo, aliwataka wahusika hao kuyatekeleza yale yote waliokusudia, kuhakikisha wanayatekeleza kwa vitendo ili kufikia malengo yake.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhani Said, alisema lengo la idara ni kuratibu shuhuli za msaada wa kisheria ili kuona wananchi wanapata huduma bora na uhakika.

Alisema idara imekua ikiyafikia makundi mbali mbali katika jamii na kuwapatia ushauri na msaada wa kisheria bila malipo, ikiwemo hata katika visiwa vidogo vidogo.

Akiwasilisha taarifa ya maadhimisho ya tatu ya Wiki ya msaada wa kisheria, mwanasheria kutoka idara ya katiba na msaada wa kisheria Ofisi ya Pemba Bakari Omar Ali, idara kwa kushirikiana na wahusika wengine wa masuala ya msaada wa kisheria na imepanga kufanya maadhimisho ya tatu.

Naye wahusika wa msaada wa kisheria, Nassor Bilali alisema kila wilaya kuwa na kambi yake katika kuelekea maadhimisho ya siku ya msaada wa kisheria.

Kwa upande wake Nassor Hakim kutoka jumuiya ya wasaidizi wa sheria Mkoani, alisema idara kutumia mbinu zaidi kwani watu wanamahitaji makubwa katika maeneo mengi.

Mwakilishi kutoka baraza la watu wenye ulemavu Pemba Ayubu Juma Shaame, alishauri katika kambi kuwepo na wakalimani wa lugha za alama, ili watu wenye mahitaji maalumu waweze kunufaika katika kambi hiyo.

MWISHO