Thursday, January 16

ZRB yawafutarisha wafanyabiashara wao Pemba

 

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor Massoud,ameungana na kamishana wa bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Musaph Juma Mwenda, katika futari maalumu waliowaandalia wafanyabiashara wa Pemba.

Akitoa neno la shukurani mara baada ya kumalizika kwa futari hiyo, kwa niaba ya kamishna wa bodi ya ZRB Zanzibar, mkurugenzi wa Utawala ZRB Pemba Jamal Hassan Jamal, aliwashukuru wafanyabiashara hao kuhudhuria katika futari hiyo.

Alisema ZRB itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara ili kuona kodi ya serikali inalipwa na wanatumia mashine za kieletroniki wakati wanapofanya malipo.

Aliwataka wafanyabiashara hao kuachana na dhana potofu walionayonayo kuwa mashine hizo zinaongeza tozo, jambo ambalo sio hahihi.

“ZRB itaendelea kuwashirikiana na wafanyabiashara muda wote na kuona zile changamoto zilizokuwepo zinaondoshwa na kila kitu kinakuwa sawa”alisema.

Alisema iwapo wafanyabiashara watatumia mashine ipasavyo basi kutolea risit, basi inchi itapata fedha kupeleka maendeleo bora na kupiga hatua.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara mara baada ya kumalizika kwa futari hiyo, katibu wa PESTA Mkoa wa Kusini Pemba Hafidh Mbarka Salim, alisema suala la ulipaji wa kodi ni suala la lazima kwa mfanyabiashara yoyote.

Alisema ZRB lazima ijenge uhusiano rafiki na wafanyabiashara, ili kila mtu aweze kufuarahi katika suala la kodi baina ya wafanyabiashara na wanaokusanya kodi.

“Niwajibu wetu kuyafanyia kazi changamoto zote zinazowakubwa wafanyabiashara, ili waweze kulipa kodi vizuri na serikali kupata mapato yake”alisema.

Hata hivyo futari hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, kamishna wa ZRB, Mwenyekiti wa bodi ya ZRB, maafisa wadhamini wa taasisi za Serikali Pemba na wafanyabiashara.

MWISHO