NA ABDI SULEIMAN.
WANAFUNZI 1090 Kisiwani Pemba, wameanza rasmi mitihani yao ya kidato cha sita katika skuli mbali mbali, huku mitihani hiyo ikifanywa katika hali ya amani na utuluvu.
Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mitihani hiyo inavyofanyika kisiwani humo, Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, alisema jumla ya vituo 12 vya serikali na vituo viwili vya binafsi vinatumika kufanywa mitihani hiyo.
Alisema maandalizi yote mazuri na wamejiandaa vizuri, ikiwemo miundombinu na maabara zote ziko vizuri pamoja na vifaa vyake vimekamilika na vyakisasa katika maabara hizo.
“Licha ya mvua kuendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba, lakini mpaka sasa hakuna skuli au darasa hata moja linalovuja, wanafunzi wako vizuri na wanafanya mitihani vizuri,”alisema.
Aidha alisema mitihani hiyo inafanywa kwa kutumia kanuni za baraza la Mitihani Tanzania, kwani wasimamizi wa mitihani hiyo ikiwemo walimu wote ni wadilifu na hakuna mwanafunzi atakae tokea kuonewa, kutokana na kujipanga vizuri katika ufanyaji wa mitihani hiyo.
Mdhamini huyo alisema imani yake hakutatokea mwanafunzi yoyote atakaejihusisha na udanganyifu katika mitihani hiyo na kupelekea kufutiwa mitihani, kutokana na maandalizi waliopatiwa kupitia Wizara ya Serikali yao.
Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuwaombea dua wanafunzi hao, ili waweze kumalizia mitihani yao kwa salama na amani, huku ufauli wakitarajia kuongezeka.
Akizungumzia suala la usafiri katika kipindi hiki cha Mvua, aliwataka madereva kuwaangalia wanafunzi kwa kuwasaidia pale wanapokwenda skuli, kwani kuna baadhi yao wanaendelea kufanya mitihani na sio kuwaacha katika vituo au maeneo kwa kutokua na nauli.
Kwa upande wa Skuli ya Utaani ambayo ilipata mitihani wa kuungua moto katika bweni la wanawake, alisema serikali ilisimamia vizuri ili kuona wanafunzi wale wanawafanya mitihani yao vizuri, kwani changamoto zote zilizokuwa zikiwakabili zimetatuliwa.
“Kilio kikubwa cha wazazi, walimu na walimu ni kuteketea kwa vifaa vyao na maabara, ila serikali ilijipanga kuhakikisha wanafunzi wa utaani wanafanya miatihani kwa kuwekwa mazingira mazuri ikiwemo vifaa vya kisasa vya maabara skuli hapo,”alisema.
Hata hivyo aliwataka wazazi kufahamu kuwa wanafunzi wa utaani, wameanza mitihani yao vizuri na vifaa vyote vinavyohitajika vipo, huku akiwasihi katika kipindi hiki kuachana na mtindo wakuomba lifti kwa kutumia bodaboda kwani baadhi yao sio waaminifu.
Kwa upnade wao wanafunzi wa skuli ya Sekondari Madungu Sekondari, Fidel Castro na Shamiani Sekondari, wamesema mitihani hiyo wameanza kuwa amani na utulivu.
Wamesema kwa siku ya kwanza hakuna kasoro yoyote iliyotokea, kwani vifaa vyote vimekamilika na wameanza kufanya kwa wakati muwafaka.
MWISHO
Wanafunzi hao walifanya mitahi katika vituo 12 vya Serikali na vituo viwili vya watu binafsi,