Wednesday, January 15

VIUONGOZI wa DIni munamchango mkubwa kuhamasiha suala la Amani

NA ABDI SULEIMAN.

ILI kuepuka migogoro ya ardhi na mirathi kuendelea kutokea, imeelezwa kwamba viongozi wa dini bado wananafasi kubwa ya kuelimisha waumini wao, ili kuzuwia migogoro hiyo kuendelea kutokea nchini.

Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Pemba Bakar Ali Bakar, alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Chake Chake, katika kikao cha kuhamasisha Mashehe na Viongozi wa Dini juu ya elimu ya mirathi kupitia majukwaa mbali mbali, mkutano ulioandaliwa na jumuiya ya PECEO.

Alisema migogoro ya ardhi katika siku za hivi karibuni imekua mingi sana, hivyo viongozi wa dini wanaweza kuwa msaada mkubwa kusaidia kama ilivyokua katika suala la uhamasishaji utunzaji wa amani na Uviko 19.

“Iwapo elimu hiyo kama itatolewa ipasavyo, basi migogoro itapungua ya ardhi na hata mirathi, na kufikia malengo yaliyokusudiwa,”alisema.

Alifahamisha kuwa, serikali inakesi nyingi katika mahakama ya ardhi, hivyo elimu hiyo itasaidia kupunguza migogoro katika mahakama za ardhi.

Aliongeza kwamba migogoro mingi inatoka katika ardhi, wakati ardhi iliyopo ni ndogo haiongezeki, huku shuhuli za kijamii na makaazi yakizidi kuongezeka pia.

Hata hivyo aliitaka PECEO kwa kutekeleza mradi huo, pamoja na kuhakikisha wanawake wanapata haki zao za ardhi na mirathi kama ilivyo kwa wanaume.

Naye Mchungaji Benjamini Kissanga, alisema wananchi ndio tatizo kwa kuchelewesha kuifikisha mirathi katika sehemu husika baada ya mmoja ya wanafamilia kufariki.

Alisema kesi zinapotokea huamuliwa katika familia, ikishindikana huenda mahakamani ili kila mtu kuweza kupata haki zake kikamilifu.

Kwa upande wake Shekhe, Iddi Haji Juma kutoka Wakfu na Mali ya Amana Pemba, alisema serikali imetaka masuala yote ya mirathi kupelekwa kamisheni ya Wakfu na Mali amana kwa ajili ya kurithisha kisheria.

Alisema katika uislamu hali ya kumiliki mali ni ya kila mmoja, ndio maana mirathi ikawa inachelewa na kupelekea wanawake kukosa haki zao, huku akibainisha kuwa mwanamke anahaki ya kupata mirathi kwa mujibu wa sheria.

“Baada ya kufariki mmoja ya wanafamilia kinachofuata ni kurithishana, ila kwanza kutolewe madeni, kuzika ndipo wanafamiliwa wanapaswa kufanya mirathi.

Katibu wa PECEO Juma Said aliwataka viongozi hao kuhakikisha elimu hiyo waliopatiwa inafikishwa kwa walengwa wao, kwani suala la mirathi na ardhi ni changamoto kubwa kwa jamii.

Naye Salma Omar Ali kutoka Wete, aliwataka wananchi wakati wanapotaka kurithishana kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni kufika wakfu na mali ya amana, ili kupatiwa hati miliki yake.

MWISHO.     

 


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1736977740): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48