Thursday, November 14

MCT LATANGAAZA MAJINA WASHINDI TUZO ZA WANAHABARI: ZANZIBAR LEO PEMBA OYEEEEEEEE.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Dar es Salaam, Alhamisi, Mei 19, 2022

Jopo la majaji saba lililokaa kwa siku tisa, kuanzia Mei 7 hadi 15, 2022 kupitia jumla ya kazi 598 za waandishi zilizokuwa katika makundi 20 ya kushindaniwa katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021, limemaliza kazi yake, Mei 15, 2022.

Jopo hilo lilitumia siku tisa badala ya nane kutokana na ongezeko la kazi 202 kutoka Tuzo za EJAT 2020, ambapo jumla ya kazi 396 ziliwasilishwa ukilinganisha na kazi 598 za sasa. Hapa niwapongeze na kuwashukuru majaji kwa kazi kubwa waliyoifanya usiku na mchana yakupitia kazi hizo.

Jopo liliongozwa na mwenyekiti, Mkumbwa Ally. Wajumbe wengine walikuwa Mwanzo Millinga (Katibu), Aboubakar Famau, Mbaraka Islam, Imane Duwe, Beatrice Bandawe, na Rose Haji, ambao waliapishwa Mei 6, 2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Robert Makaramba.

Majaji hao wameteua jumla ya waandishi 60 ambao kazi zao zimeonekana kuwa bora Zaidi na ambao miongoni mwao watapatikana washindi wa EJAT 2021.  Kati ya wateule hao, wateule tisa wanaandikia runinga; 12 vyombo vya mtandaoni, wanane redio na 31 wanaandikia magazeti.

Idadi ya wateule wa EJAT 2021 kwa upande wa wanawake ni 28 ambayo ni asilimia 47 ikiwa ni ongezeko la asilimia tatu kulinganisha na Tuzo zilizopita ambapo wanawake walikuwa 26 sawa na asilimia 44 ya walioingia kwenye hatua hii mwaka jana. Wateule wanaume ni 32, sawa na asilimia 53.

Kati ya wateule 28 wanawake, 18 wanatoka katika magezeti, runinga wametoka watatu, radio wawili na vyombo vya habari vya mtandaoni watano. Kwa upande wa waandishi wa habari wanaume, magazeti wametoka 12, runinga waandishi sita, radio wateule sita na vyombo vya habari vya mtandaoni wateule saba.

Kwa mujibu wa majaji wa EJAT 2021, kazi za mwaka huu, zimeonyesha kuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na mwaka jana. Hii ni pamoja na kiwango cha waandishi wa habari wa vyombo vya mtandaoni kuonyesha kukomaa zaidi katika kazi zao na mwamko wa ushiriki katika Tuzo hizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika shughuli za utoaji Tuzo na ndiye atakaye mkabidhi Tuzo mshindi wa jumla pamoja na mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa Habari  (LAJA) 2022.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mei 28, 2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Hii itakuwa ni mara  ya 13 kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi katika mwaka uliotangulia.


Baraza linapenda kuwataarifu waandishi wa habari kuwa katika Tuzo za mwakani, mfumo wa ujazaji fomu utakuwa ni kwa njia ya mtandao (online) ambapo fomu zitajazwa na kutumwa kwa mtandao. Hii itapunguza matumizi ya karatasi na changamoto za CD kukwama kucheza wakati majaji wanapitia kazi.

Taasisi zinaounda Kamati ya Maandalizi ni pamoja na MCT, Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu, Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Misa-Tan na Twaweza.

Tuzo hizi zinafadhiliwa na Wajibu Institute, Natural Resources Governance Institute (NRGI), Bank ABC, Hakielimu, Tume ya Ushirika, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Busota Inn, Serena Hotel Dar es Salaam, Coca Cola, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Azam Media, Twaweza na COSTECH.

Makundi yanayoshindaniwa katika Tuzo za EJAT 2021 ni:-

  1. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha;
  2. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni;
  3. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo;
  4. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu;
  5. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi;
  6. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi;
  7. Tuzo za Uandishi wa Habari za Data;
  8. Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu
  9. Tuzo za Uandishi wa Habari za Utawala Bora na Uwajibikaji;
  10. Mpiga Picha Bora – Magazeti;
  11. Mpiga Picha Bora – Runinga;
  12. Mchora Katuni Bora;
  13. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto;
  14. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini;
  15. Tuzo za Uandishi wa Habari za Walemavu;
  16. Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya;
  17. Tuzo ya Uandishi wa Sayansi na Teknolojia;
  18. Tuzo za Uandishi wa Habari za Hedhi Salama;
  19. Tuzo za Uandishi wa Habari za Ushirika; na
  20. Kundi la Wazi.

Ifuatayo ni orodha ya wateule wa EJAT 2021 pamoja na vyombo vyao 

 

SN NOMINEES MEDIA OUTLETS
1 Mariam Shabani Mbwana Mwananchi
2 Tumaini Godwin Msowoya Mwananchi
3 Peter Simon Rodgers ITV
4 Agusta Mathias Njonji Nipashe
5 Nusra Shaaban Kichongapishi TIFU TV- Online
6 Adam Gabriel Hhando CG FM Radio
7 Haji Nassor Mohamed Zanzibar Leo
8 Khamisuu Abdallah Ali Zanzibar Leo
9 Naishooki Alais Makaseni STAR TV
10 Sanula Renatus Athanas Nipashe
11 Lugendo Ibrahim Madege UFM Radio
12 Anthony Mayunga Mayunga Mwananchi
13 Ephrahim Edward Bahemu Mwananchi
14 Maryam Salum Habib Zanzibar Leo
15 Said Seleman Lufune City FM
16 Pascal Michael Buyaga TBC1
17 Aurea Simtoe Mwananchi
18 Salum Vuai Issa Zanzibar Leo
19 Masekepa Natisa Masekepa ITV
20 Sabato Mafwiri Kasika Nipashe
21 Muhidin Ally Msamba The Guardian
22 Amina Ahmed Mohamed Zanzibar Leo
23 Harith Jaha Ally Watetezi TV – Online
24 Gladness Joseph Msetti UFM RADIO
25 Zuhura Hassan Makuka Dar 24 (Online)
26 Jackline Inyas Silemu ITV
27 Francis Dhamira Kajubi The Guardian
28 Isakwisa Njole Mbyale Highlands FM radio
29 Harieth Isaya Makweta Mwananchi
30 Halfan Chusi Nipashe
31 Khalifa Said Rashid The Chanzo – Online
32 Irene Nicholaus Mwasomola Uhuru
33 Elizabeth Edward Kusekwa Mwananchi
34 Baraka Jailos Messa Habari Leo
35 Martha Stephen Nalimi Shamba FM
36 Joyce David Joliga The Citizen
37 Mariam Ngollo John Nukta.blog
38 Najjat Haji Omar The Chanzo – Online
39 Salma Msichoke Mrisho STAR TV
40 Peter Lugendo John TBC FM
41 Beatrice Philemon Mukocho The Guardian
42 Joe Beda Rupia Jamhuri
43 Hanifa Salim Mohamed Zanzibar Leo
44 Amour Khamis Ali Zanzibar Cable TV
45 Abdi Juma Seleman Zanzibar Leo
46 Protte Profit Mmanga LEO TV – Online
47 Faraja John Sendegeya Azam TV
48 Festo Charles Lumwe Dar 24 – Online
49 Mary Geofrey Mashina Nipashe
50 Munira Abdillah Hussein BBC Swahili (Online)
51 Daniel Samson Nukta.habari blog
52 Habiba Zarali Rukuni Zanzibar Leo
53 Marco Zephania Maduhu Nipashe
54 Christina Stephen Mwakangale The Guardian
55 Elizabeth Cornery Zaya Nipashe
56 Sudi Shaban Ally STAR TV
57 Omary Hussein Omary STAR TV
58 Jecha Simai Jecha ZBC FM
59 Jenifer Julius Gilla The Guardian
60 Lukelo Francis Haule The Chanzo- Online

——————————–

Kajubi D. Mukajanga 

Mwenyekiti

Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2021