NA ABDI SULEIMAN.
AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu SMZ Pemba Thabit Othaman Abdalla, amesema kuzinduliwa kwa Muongozo wa Upatakanaji wa Msaada wa kisheria vizuwizini, Muongozo wa uanzishwaji wa vituo vya msaada wa kisheria katika Vyuo vikuu na vituo vinavyotoa mafunzo ya sheria, inalengo la kuleta haki, amani na stahiki ya nchi.
Alisema miongozo hiyo inapelekea kupatikana kwa haki na upatikanaji wa malengo endelevu katika nchi, kwani hata viongozi wa kuu wa taifa wamekuwa ni wahubiri wakubwa wa suala la amani.
Aidha alisema lazima haki na stahiki za wananchi zipatikane, kwani hawawezi kuzungumzia amani na utulivu bila ya kuzungumzia suala la haki.
Mdhamini Thabit aliyaeleza hayo katika hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Upatokanaji wa Msaada wa kisheri vizuwizini na Muongpozo wa uanzishwaji wa vituo vya msaada wa kisheria katika Vyuo vikuu na vituo vinavyotoa mafunzoi ya sheria, inalengo la kuleta haki, amani na stahiuki ya nchi.
Alisema katiba ya Zanzibar imesisitiza watu wote ni sawa na wanahaki sawa na kupata stahiki zao kikamilifu, hata mikataba kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia na inahimiza usawa.
“Rais wetu amekuwa ni muumini mkubwa wa masuala la amani, haki na stahiki za watu kupatikana, lazima na sisi wasimamizi wa sheria tuhakikishe miongozo hii inafuatwa kikamilifu,”alisema.
Aidha alisema serikali kupitia idara ya katiba na msaada wa kisheria Zanzibar, imekua ikishuhudia malalamiko mengi katika suala la sheria, hivyo kuwepo kwa miongozo hiyo changamoto hiyo itaweza kutatuka.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utalawa Bora Halima Khamis Ali, alisema idara ya katiba na msaada wa kisheria Zanzibar imekua inaratibu masuala msaada wa kisheria kwa kuwapatia wananchi wanaohitaji huduma hiyo.
Alisema watoaji wa huduma na wasimamizi wataweza, kuifahamu miongozo na kuifanyia kazi pamoja na kuitekeleza kikamilifu kama lengo lililokusudiwa.
“Miongozo hii itakuwa chachu ya upatikanaji wa haki, pale panapokua na changamoto sasa itakuwa ni basi kwa changamoto hizo”alisema.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema uletekelezaji wa mradi huu wa upatikanaji wa haki kupitia kwa LSF, huku akiwapongeza wafadhili hao kupitia shirika hilo.
Alisema lengo ni kutoa uwelewa kwa wahusika wa haki na wasimamizi wa sheria, huku akiwataka wasimamizi hao wa sheria kuhakikisha wanashirikiana baina ya watoaji wa masaada wa kisheria na wasimamizi wa sheria.
Kwa upande wao wasimamizi hao, wamesema kuzinduliwa kwa miongozo hiyo itaweza kuwasaidia wananchi kupata haki zao za kisheria, ambazo wamekuwa wakizikosa muda mrefu.
MWISHO