NA KHADIJA KOMBO,PEMBA
Watu wenye mahitaji maalum Kisiwani Pemba wameishukuru Jumuiya ya maendeleo ya Kimataifa Zanzibar ZIDO kwa kuwapatia vifaa vya usaidizi ambavyo vitawarahisishia katika kufanya shughuli zao mbali mbali za kijamii.
Wakizungumza mara baada ya kupewa msaada huo wamesema kukosekana kwa vifaa hivyo kwao kuliwawiya vigumu kushirikiana na wanajamii wenzao katika harakati mbali mbali za kijamii.
Kwa upande wake Mtendaje Mkuu wa Jumuiya hio kwa upande wa Zanzibar ndugu Makame Ramadhan amesema ZIDO wakati wote imekuwa karibu na wananchi katika kusaidia kuondoa kero mbali mbali zinazo wakabili kwani kufanya hivyo ni moja kati ya kuiunga mkono Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi zake za kuinua wananchi kiuchumi.
Naye Mrajis wa Jumuiya zisizo za kiserikali Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla amesema ZIDO ni jumuiya inayofaa kupongezwa kutokana na juhudi zake katika kuondoa shida kwa wanajamii hususan wenye mazingira magumu hivyo amezitaka jumuiya yengine kuiga mfano huo.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na fimbo nyeupe kwa wasioona, vigari vya magurudumu matatu pamoja na chakula ikiwa ni pamoja na mchele, unga wa ngano, maharage, Mafuta ya kupikia na sukari ambapo pia katika hafla hio ZIDO ilipata nafasi ya kula chakula cha mchana pamoja na wanajamii hao.
Mwisho.
KUANGALIA VIDEO YA HABARI HII BONYEZA HAPA
<code>