NA ABDI SULEIMAN.
SKULI ya sekondari Kiwani Imefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza kwa kupata asilimia 70%, katika mashindano ya chemsha bongo ya Ukimwi, mashindano hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), yakiwa na lengo la kutoa uwelewa kwa wanafunzi juu ya masuala mbali mbali ya VVU na Ukimwi.
Nafasi ya Pili ikachukuliwa na skuli ya Amini Sekondari kutoka Wesha iliyopata 66%, nafasi ya tatau ikaenda kwa skuli ya Chwale Sekondari iliyopata alama 63%, nafasi ya nne ikiwenda kwa skuli ya Shumba Sekondari, Uwandani sekondari nafasi ya tano na sita ikaenda kwa skuli ya Mwitani Sekondari.
akizungumza na wanafunzi hao Mjini Chake Chake, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Ahmed Aboubakar, aliwataka walimu kuziimarisha klabu za UKIMWI katika skuli zao, ili elimu hiyo iweze kuwafikia wanafunzi waliowengi.
Alisema wananchi wanapswa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi Ukimwi, kwani mikakati ya ZAC kufika 2030 kusiwe na maambukizi mapya ya Ukimwi na waliona maambukizi wanaendelea kutumia dawa za ARV ipasavyo.
“Ukimwi Upo na hawajuwi lini utakwisha, mapambano yanaendelea ni wakati sasa kwa wazazi kuendelea kuelimisha wananchi juu ya kupiga vita maambukizo mapya,”alisema.
Aidha aliwataka vijana kujitahidi kua wawazi, kuangalia thamani yao kwani maradhi ya ukimwi sio sababu ya kuondoka mapema, hivyo lazima kutunza thamani yao.
Naye Sihaba Saadat kutoka Tume ya Ukimwi Zanzibar, alisema bado uwelewa wa vijana ni Mdogo katika suala la UVV, hali iyopelekea kwenda ana kwa ana hadi kuwafikia vijana.
Kaimu Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar, alisema tume ya ukimwi imelazimika kushirikiana na Wizara ya Elimu katika kuwajengea uwelewa wanafunzi juu ya masuala mbali mbali ya Ukimwi.
Kwa upande wake Dkt.Amour Rashid, aliwataka wanafunzi hao kutambua thamani yao, kwani bahati walioipata wao ni lulu na kutambua kuwa wanao ni wawakilishi wa skuli zilizobakia.
Alisema juhudi zinazotolewa na ZAC zinasaidia sana Wizara ya ELimu katika kutengeneza mitaala, ambayo inatumika katika kuwafundishia wanafunzi.
MWISHO